KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, October 8, 2013

Rais Paul Biya wa Cameroon amrejesha Samwel Eto'o uwanjani kimataifa kama aliavyofanya kwa Roger Milla.

Rais wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mshambuliajhi Samuel Eto'o kufikiria kwa mara nyingine juu ya maamuzi yake ya kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya  Chelsea alikutana na wawakilishi wa Rais Biya jijini Yaounde wakijadili juu ya hatima ya baadaye ya mshambuliaji huyo.
Baada ya kukutana hatimaye Eto'o, amekubali kurejea kuitumikia tena Cameroon.
Sasa anatarajiwa kusafiri kuelekea Ufaransa kujiunga na kikosi cha timu hiyo ambacho kinajiandaa kwa ajili ya mchezo wa hatua ya mwisho kusaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia wakikabiliwa na mchezo dhidi ya Tunisia.
Eto'o mwenye umri wa miaka 32 hapo kabla aliwaambia wachezaji wenzake kuwa hana nia ya kuendelea kuitumikia Cameroon kauli ambayo aliitoa baada ya mchezo dhidi ya Libya ambao walishinda na kusonga mbele katika hatua ya mwisho ya mtono.
Licha ya taarifa za kujiondoa kikosini, bado kocha wa kikosi hicho Volker Finke ameendelea kumtaja mchezaji huyo katika kikosi chake kitakacho vaana na Tunisia kwani alikuwa bado hajawasilisha taarifa rasmi ya tangazo lake hilo.
Eto'o amekuwa hana mahusinao mazuri na mamlaka ya soka ya nchi yake tangu huko nyuma ambapo akiwa nahodha aliongoza mgomo wa kudai posho kiasi hata kuvuruga mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria mwaka 2011.
Tukio hilo lilipelekea kufungiwa kwa michezo 15 kabla ya adhabu hiyo kupunguzwa na kuwa miezi minane.
Hii si mara ya kwanza kwa Rais Biya kukatisha majaribio ya kustaafu kwa wachezaji, kwani aliwahi kufanya hivyo kwa Roger Milla ambaye alirejea dimbani katika fainali za kombe la dunia mwaka 1990 nchini Italia.

No comments:

Post a Comment