KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 30, 2013

Kombe la dunia: Ronaldo de Lima anasema hakuna anayetaka kukutana na wenyeji Brazil.

The legendary Selecao star Ronaldo de Lima anasema hakuna kikosi hata kimoja ambacho kinapenda kukutana na kikosi cha Scolari kwenye fainali ya kombe la dunia.

Rekodi ya Selecao inaonyesha kuwa wameshinda jumla ya michezo 12 katika michezo yao ya mwisho 13.
 
Ronaldo ambaye ndiye mfungaji mwenye rekodi ya kufunga mabao mengi katika kombe la dunia ambaye aliitumikia Brazil kwa michezo 98 na kushinda makombe mawili ya dunia anaamini kuwa hakuna anayetaka kukutana na Brazil kwenye fainali hizo ambazo Brazil watakuwa nyumbani kwenye ardhi yao 2014.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Barcelona, Inter Milan, AC Milan na Corinthians ametanabaisha kuwa hana shaka na kuvunjwa kwa rekodi yake ya ufungaji wa mabao ya magoli 15 ambayo inanyemelewa na mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose na kusisitiza kuwa rekodi zinakuwepo ili zivunjwe.

“Sina hofu na hilo”
Kwasasa Klose mwenye umri wa miaka 35 ana mabao 14 akihitaji goli moja kulingana na Ronaldo De Lima.

“Every record was made to be broken. So, just as I broke a record that stood for many years, I'm sure one day mine will also be broken. It will not erase my 15 goals from history.”

No comments:

Post a Comment