KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 30, 2013

CECAFA CHALENJI CUP: KENYA YAIFYATUA SUDANI KUSINI.

Kikosi cha timun ya taifa ya Kenya kimeshinda mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi katika michuano ya Chalenji ya CECAFA dhidi ya Sudani Kusini kwa mabao 3-1 ukiwa ni mchezo wa kundi A uliopigwa katika dimba la Nyayo jijini Nairobi.
Wenyeji wa michuano hiyo Kenya ni kama wamemkaribisha kocha wao Adel Amrouche ambapo mpaka timu hizo zinakwenda kupumzika Kenya walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Penati ya Jockins Atudo baada ya dakika 16 za mchezo pamoja na goli la Jacob Keli yaliwapa uongozi Harambee Stars mpaka mapumziko. 
Nahodha wa Sudani kusini Richard Jistin alifunga goli zuri la mpira wa adhabu ya moja kwa moja kunako dakika ya 27 ambalo lilikuwa ni goli la kusawazisha kabla ya Kenya kuandika bao la pili ambapo Allan Wang alifanya juhudi binafsi kwa kutokuchelewa kuupiga mpira na mlinda mlango Juma Jinaro mlinda mlango wa Sudan kusini asijue nini cha kufanya.
David Owino, ambaye goli la mwisho kuifungia Kenya ilikuwa ni katika mchezo dhidi ya Namibia kusaka tiketi ya kombe la dunia alikandamiza msumari wa mwisho kunako dakika ya 78.

Mwamuzi wa mchezo huo kutoka Zanzibar, Waziri Sheha alimudu mchezo aliwazawadia penati wenyeji ambayo ilipigwa na Jockins Atudo na kukosa goli baada ya JacoB Keli kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Sudani kusini Juma Jinaro.
Hata hivyo Waziri Sheha alishindwa kumuadhibu mlinda mlango kwa kosa hilo na hivyo kuibua maswali juu ya maamuzi yake.

Kenya:
Duncan Ochieng, David Ochieng Owino, James Situma, Abud Omar, Jockins Atudo, Peter Opiyo, Francis Kahata (Captain), Anthony Akumu, Noah Keli, Allan Watende Wanga
Subs: Fredrick Jerim Onyango, David Geteri, Clifton Miheso, Paul Muigai Kiongera, Muligai Ndetto, Edwin Lavasta, David King’atua and Musa Mohamed
Coach: Adel Amrouche (Belgium)
South Sudan:
Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip Delfino, Fabiano Lako, Richard Jistin, William Offiri, Jimmy Eresto, Dominic Aboi, Lodule Lako, Wol Bol Yor, James Joseph
Subs: Keneddy Saturlino, Edomon Amadeo, Lubari  Zariba, Godfrey Peter, Achiul Akol, Clement Badru and Francis Khamis

No comments:

Post a Comment