Dereva wa Timu ya magari ya McLaren, Lewis
Hamilton alijikuta katika sayari yake mwenyewe kwa kuongoza mbio za magari ya
Hungary hadi mwisho.
Dereva huyo
Muingereza aliweza hata kuweka kasi ya kupindukia kwenye mizunguuko miwili,
iliyomuwekea mda wa kuweka pengo la sekunde 0.413.
Dereva wa
magari ya Lotus Romain Grosjean alifuata wa pili mbele ya Sebastian Vettel wa
timu ya magari ya Red Bull.
Muingereza
Jenson Button wa magari ya McLaren alimaliza wa nne, Kimi Raikkonen wa 5,
Fernando Alonso akamaliza wa 6 huku Mark Webber akimaliza wa 11.
Nafasi ya 10
ilifunikwa na Felipe Massa wa magari ya Ferrari aliyefuatiwa na Pastor
Maldonado wa timu ya magari ya Williams akafuata Bruno Senna, na Nico
Hulkenberg wa kikosi cha Force India.
Hamilton
alisema baada ya mbio kuwa: "ni afuweni kubwa kuona matunda ya marekebisho
tuliyoyafanya na nimefurahishwa kuona kwamba nimelitumia gari ninavyotaka.
Uwezo wa
magari ya Ferrari leo umedhihirisha kuwa magari yao hayana kasi kuyashinda
mengine wakati wa ukame, na hilo limepunguza tofauti ya pointi za Dereva Alonzo
34 kutokana na kasi ya magari ya Ferrari yanayofanya vyema wakati wa mvua.


No comments:
Post a Comment