KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 29, 2012

WACHEZAJI YANGA WAJAZWA MAFEDHA.


 
Ushindi wa mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Kagame Dar es salaam Yanga  Afrika  dhidi ya Azam Fc hapo jana jumamosi  umelezwa kuwa ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na Mweyekiti wa Klabu hiyo Yusuph Manji .
Akizungumza na Rockersport Mmoja wa watu waliokuwa karibu na kambi ya yanga amesema , siku moja kabla ya mchezo huo yaani ijumaa asubuhi Manji akifuatana na viongozi  wenzake wa klabu waliwatembelea wachezaji katika kambi yao kwenye Hotel ya Double Tree iliyopo Masaki nje kidogo ya jijiji la Dar es salaa, awali wachezaji wa yanga walikuwa wakiishi kwenye hotel ya Valley View iliyopokaribu kabisa na makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya jangwani.
Imeelezwa kuwa  baada ya Manji na msafara wake kufika hotelini hapo , waliweza kuzungumza na makocha pamoja na wachezaji na katika mazungumzo hayo Manji aliwauliza wachezaji  bingwa wa michuano ya kombe la Kagame anapata nini ?
 
Wachezaji walimjibu anapata dola elfu 30, kutokana na kauli ya wachezaji,  Manji aliwaambia kuwa endapo watafanikiwa kuutwaa ubingwa huo basi pesa zote ziwe mali yao naye  akawaahidi kuwaongezea milioni kumi na tano kama zawadi yake kwa wachezaji endapo watatwaa ubingwa.

Kama haitoshi Manji pia akawaambia viongozi wenzake nao watoe ahadi zao kwa wachezaji ambapo  nao wakatoa ahadi mbali mbali za fedha na kisha msafara huo ukaondoka .

Kutokana na hali hiyo imeelezwa morari ya wachezaji na benchi zima la ufundi ikapanda zaidi na kila mchezaji akaahidi kuwa endapo atapata nafasi ya kucheza fainali hiyo atapigana kufa na kupona kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa na juhudi zao zikaisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao  2 - 0 dhidi ya Azam hivyo Yanga kwa mwaka wa pili mfululizo kutangazwa kuwa mabingwa wa michuano ya kombe la Kagame.
Kwasasa wachezaji wa Yanga wamekwenda mapumziko na watarejea kambini ijumaa kuendelea na mazoezi.
 

No comments:

Post a Comment