Mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer akijaribu kuushikilia mpira kwa lengo la kupoteza muda baada ya kufungwa bao la pili. |
Arsenal imeshindwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya licha ya kupata ushindi wa ugenini mabao 2-0 dhidi ya kigogo cha nchini Ujerumani Bayern Munich katika mchezo uliopigwa katika dimba la Allianz
Arena nchini Ujerumani.
Olivier
Giroud ndiye aliyekuwa kuwapa faraja mashabiki wa Arsenal kunako dakika ya tatu ya mchezo.
Laurent Koscielny akaandika bao la pili katika dakika za mwisho mwisho za mchezo wa mchezo hata hivyo safari ya washika mitutu hao ikaishia hapo kufuatia faida ya bao la ugenini walilopata Bavarians katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Emirate.
Laurent Koscielny akifunga bao la pili.
Olivier Giroud akifunga bao la mapema kunako dakika ya tatu.
Thomas Rosicky akipigwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Arjen Robben.
Javi Martinez (kulia) akiudonyoa mpira kuharibu mipango ya Mikel Arteta.
Mario Mandzukic akionekana kushangaa maamuzi ya mwamuzi.
Bosi wa Arsenal Arsene Wenge akilalamika kwa mwamuzi wa pembeni juu ya maamuzi ya mwamuzi wa kati.
Wenger akipiga kelele kupinga maamuzi ya mwamuzi wa kati.
Luis Gustavo (kilia) akipambana na Santi Cazorla katika ya uwanja.
Thomas Muller naye akimlalamikia mwamuzi wa pembeni kipindi cha kwanza.
Arjen Robben akichotwa na Kieran Gibbs.
Kiungo wa zamani wa Bayern Owen Hargreaves alikuwa ni mmoja wa watazamaji katika dimba la Allianz Arena.
No comments:
Post a Comment