KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 2, 2013

LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA JE YANGA KUENDELEZA MAKALI YA UTURUKI KWA MTIBWA?

Yanga na Mtibwa Sugar zinashuka dimbani leo katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itakuwa ikishuka dimbani katika mchezo huu wa pili tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikiwa vinara wa msimamo wa ligi wakiwa na alama 32 ilihali Mtibwa wakiwa katika nafasi baada ya kujikusanyia alama 22.

Endapo Yanga itashinda katika mchezo wa leo itakuwa inafikisha alama 35 ambazo zitiaifanya kuzidi kutanua utofauti mwanya wa alama kati yake na Azam yenye alama.

Mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.

Mchezo mwingine hii leo ni kati ya Polisi Morogoro na African Lyon utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani.  
Jijini Tanga kutakuwa na mchezo mwingine ambapo Mgambo Shooting watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.

Kesho (Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment