Mzunguko wa pili wa pili daraja la kwanza(FDL) unaanza leo ambapo Villa
Squad na Moro United zitakuwa zikiumanau katika uwanja wa
Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa lala salama.
Kundi
A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa
Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa
Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mechi
nyingine ya Kundi B itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja
wa Mabatini mkoani Pwani. Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT
(Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto,
Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora
na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Ligi
hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi
wa kila kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
No comments:
Post a Comment