Bado haijulikani kama mchezaji
matata wa Real Madrid Gareth bale atacheza katika mechi dhidi ya
Liverpool katika ligi ya mabingwa ulaya hapo Jumatano.
Bale mwenye
umri wa miaka 25 anauguza jeraha la misuli ya paja. Jeraha hili
lilimpelekea kutoshiriki mechi ya Real madrid dhidi ya Levante Jumamosi
licha ya kuratibiwa kama mchezaji wa ziada.
Taarifa iliyotelewa
na Real Madrid haikufafanua muda ambao Bale atasali nje ya uwanja hata
hivyo walisema atazidi kukaguliwa jinsi anavyopata nafuu.
Baada ya
mechi yao ya Kundi B itakayochezewa ugani Anfield, Real Madrid
inatarajiwa kukabana koo na mahasimu wao wa jadi Barcelona katika ligi
ya El Clasico hapo jumamosi.
Bale aliichezea timu yake ya taifa ya
Wale kwa vipindi vyote viwili dhidi ya Bosnia Hercegovina hapo tarehe
10 oktoba na kisha akaichezea tena dhidi ya Cyprus siku tatu zilizofuata
katika michuano ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa ulaya.
Bale ambaye
alihamia Real Madrid kutoka Tottenham mwaka uliopita kwa kima cha
takriban pauni milioni 85.3, ameichezea real Madrid mechi 12 huku akiwa
amefunga mabao matano
No comments:
Post a Comment