Zacharia Hans Poppe akiongea na mwandishi wa habari wa redio EBONY FM Zainab Kiluwale ofisini kwake Tangibovu maeneo ya Mbezi beach leo akithibitisha kukabidhi barua ya kujiuzuru uongozi Simba. |
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Zackaria Hanspop ameamua kumwaga manyanga na kuachana na klabu hiyo kufuatia kile alichokisema mwenyewe kuwa ni kutokana na kuona mambo yanakwenda mrama ndani ya klabu hiyo.
Akiongea na kipindi na michezo na burudani cha Ebony fm Iringa, Hanspop amesema maamuzi yake hayo ni kuwajibika kwa nafasi yake jambo ambalo linaweza kufanywa na kiongozi yoyote anapoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo katika klabu na kuamua kuachana na nafasi yake.
Hans Pop amesema anaamini uongozi wa Simba ndio ulio ifikisha klabu hiyo hapo ilipo sasa na kwamba yeye ameona kwa busara alizonazo bora kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi.
Amesema ataendelea kuwa mwanachama mtiifu wa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa katika kundi mashuhuri rafiki la klabu hiyo la Frends of Simba kwa lengo la kuendelea kutoa mchango wake ndani ya klabu hiyo.
Taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geoffrer Nyange Kaburu naye amemwaga manyanga kuongoza Simba. Taarifa zaidi stay tune.........
BOFYA CHINI KUMSIKILIZA HANSPOP
No comments:
Post a Comment