Sylvester Kirwa |
WAKENYA KUCHEZESHA MECHI YA STARS, ZAMBIA
Mwamuzi
Sylvester Kirwa kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya
kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Kirwa
anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range. Waamuzi hao wasaidizi ambao
vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini
hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa
kuwa na msisimko wa aina yake.
No comments:
Post a Comment