Mfungaji anayeongoza katika klabu ya West Ham Diafro Sakho imeelezwa kuwa yuko fiti kuelekea katika mchezo wa Jumamosi wa Premier League dhidi ya Aston Villa baada ya kuponya majeraha yake ya bega.
Sakho alikutana na tatizo hilo katika dakika za mwisho kabisa za mchezo wa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Manchester
City mwezi uliopita ambapo aliukosa pia mchezo wa jumamoso iliyopita dhidi ya Stoke
City.
Lakini hata hivyo mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa hivi karibuni ambaye amekuwa akifunga karibu kila mchezo wa ligi kuu kwasasa yuko fiti kukichezea kikosi cha meneja Sam Allardyce's watakapo kuwa safarini Villa Park.
Allardyce pia anategemea kuwa na Winston Reid baada ya mlinzi huyo kutolewa katika mchezo dhidi ya Stoke,
licha ya kumkosa Guy Demel mwenye matatizo ya paja.
No comments:
Post a Comment