Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa Aleksandar Kolarov atakosekana katika kipindi cha takribani mwezi mzima kufuatia matatizo ya msuli.
Mlinzi huyo alipatwa na majeraha katika maandalizi ya kupasha misuli joto kabla ya mchezo dhidi ya Manchester Jumapili iliyopita na nafasi yake kuchukuliwa na Gael Clichy kabla ya kukabiliana na kikosi cha Louis
van Gaal.
Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia sasa atakuwa katika kipindi mapumziko ingawa Pellegrini kuwa mlinzi Eliaquim
Mangala atakuwa safi katika mchezo dhidi ya CSKA Moscow.
"Kolarov alipatwa na matatizo ya msuli atakuwa nje kwa mwezi mzima" amewambia waandishi wa habari "Mangala atakuwepo katika orodha ya wachezaji katika mchezo wa kesho."
No comments:
Post a Comment