KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 4, 2013

CARLO ANCELOTTI ANASISITIZA KUWA KARIM BENZEAM NDIO CHAGUO LAKE NAMBA MOJA LICHA YA KUSHINDWA KUZIFUMANIA NYAVU HIVI KARIBUNI.

 Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa Karim Benzema atasalia kuwa mshambuliaji wake namba moja kikosini licha ya kufanya hovyo mbele ya goli katika michezo ya wiki za hivi karibuni. 

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Olympique Lyonna ameshindwa kufunga katika michezo mitano ya ligi ya Hispania  La Liga na amekuwa akipigiwa filimbi mara kadhaa na mashabiki wa Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Kama hiyo haitoshi , Ancelotti anaridhishwa kiwango cha mshambuliaji huyo na kwamba hana nia ya kumshuka kutoka kikosi cha kwanza hivi karibuni

Amenukuliwa akisema 
"Benzema ana nafasi yake ndani ya kikosi na atasalia katika kikosi cha kwanza " Bosi huyo wa Blancos ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari .

"Hajafunga katika michezo mitano iliyopita lakini bado nina imani naye. Sijaongea naye baada ya mchezo wa mwisho kwakuwa hataki kufanya hivyo."

Pia kocha huyo mtaliano akaenda mbali zaidi kwa kumjaza misifa Angel Di Maria kwa kiwango safi mpaka sasa tangu kuanaza kwa msimu.

Pia Ancelotti amemzungumzia mlinzi wake wa kati Raphael Varane baada ya kurejea kutoka katika majeruhi akisema kuwa kurejea kwake kutaongeza ushindani katika sehemu ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment