|
Naibu
Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye (kushoto) akimpa mkono nahodha wa
timu ya Polisi, Makame Ally (kulia) wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji
wanaokwenda kwenye mashindano ya polisi kwa nchi zilizopo Kusini mwa jangwa la
Sahara (SAPCCO) iliyofanyika Chuo cha Maafisa Polisi, Kilwa road leo. |
|
Wanamichezo wa kiume wakimsikiliza mgeni rasmi. |
|
Wanamichezo waanawake wakimsikiliza mgani rasmi |
|
Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye akizungumza wakati akiwaaga wanamichezo |
|
Wanamichezo wakiwa pamoja na maofisa wa polisi |
WANAMICHEZO wa jeshi la Polisi Tanzania wanaokwenda kwenye michezo ya
polisi kwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SARPPCO) wameagwa
leo na Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye na kutahadharishwa kujilinda na ugongwa wa UKIMWI ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi bendera Naibu
Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye alisema lengo la michezo
hiyo ni kuwafanya wafahamiane na polisi wa nchi zingine pia
kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu.
Timu
zinazokwenda kwenye mashindano hayo ni soka, mpira wa pete (netboli)
darts na riadha ambapo wanamichezo 67 ndio waliokwenda.
No comments:
Post a Comment