Mwakilishi wa wanachama wa Coastal Union,Salim Al Mazrui |
MKUTANO
mkuu wa dharura wa wanachama kumjadili aliyekuwa Mwenyekiti wa Coastal
Union Hemed Aurora kujiuzulu unatarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii kwenye
ukumbi wa Makao makuu ya Klabu ya Coastal Union barabara 11 jijini Tanga.
Mkutano
huo unatarajiwa kuanza saa nne asubuhi utakaohusisha wanachama hai ambao wamelipia
kadi zao na hawadaiwi madeni yoyote.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Mwakilishi wa Wanachama wa Coastal Union,Salim Al-Mazrui
alisema maandalizi ya kuelekea mkutano huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na
utakuwa na agenda mbili muhimu zitakazojadiliwa.
Al
Mazrui alisema agenda ya kwanza itakuwa ni kujadilia uvumi uliojitokeza wa
kujadili kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union, Hemed
Hilal Aurora.
Alisema
agenda ya pili itakuwa ni kujadili utendaji wa Makamu Mwenyekiti wa Coastal
Union Steven Mguto ndani ya klabu hiyo hasa kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu
Tanzania bara na kutoa maamuzi.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Coastal Union ya Hemed Aurora |
Mwakilishi
huyo aliwataka wanachama wa Coastal Union waliokuwa hai kuhakikisha
wanajitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wenye lango pia la kuangalia namna ya
kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kuu.
Kwa
upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alithibitisha kupokea
taarifa ya mkutano huo na hivyo utafanyika siku ya Jumapili kutokana na
wanachama hao kufuata taratibu zote.
No comments:
Post a Comment