BAADA ya klabu ya Simba kuachana na kocha wake Milovan Circkovic ambaye ameikacha klabu hiyo bila sababu za kueleweka, taarifa za ndani za awali zinasema klabu hiyo imeamua kumuajiri kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain na Asec Memosas ya Ivory coast ambaye ni raia wa Ufaransa.
Patrick
Liewig aliyezaliwa mwaka 04/10/1950 kwasasa akiwa na umri wa miaka 62 ndiye kocha mtarajiwa wa wekundu hao wa Msimbazi na anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa kuanza kibarua hicho.
Uchunguzi wa Rockersports umebaini kuwa kocha huyo atakuwa ndiye kocha mwenye mshahara mkubwa kuliko makocha wote wa kigeni walioko nchini kwasasa wakifundisha vilabu mbalimbali vya ligi kuu.
Kwasasa atakuwa anatokea katika klabu ya El Gawafel Sportives de
Gafsa(EGS) inayoshiriki ligi kuu ya Tusia ambako alimwajiri tarehe 20.10.2012
na kudumu nayo kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kabla ya
hapo alitokea katika klabu ya MC Algier ya Algeria ambako aliajiriwa kama
meneja 01/07/ 2012 ambako pia alidumu kwa mwezi mmoja kabla ya kuelekea EGS
Gafsa).
Ni kocha
mzoefu katika soka la Afrika licha ya kufundisha zaidi timu za Tunisia ambapo
alifundisha pia Club Africain ya Tunis kuanzia
19/04/2012 mpaka 30/06/2012 akiwa kama kocha wa muda pia amewahi
kuifundisha Stade Tunisien ya Tunisia kuanzia 01/07/2009 mpaka 22/07/2011 kama
meneja.
Kocha huyu
amekuwa katika kipindi cha mafanikio zaidi katika kazi yake ya ufundishaji soka katika klabu ya ASEC Mimosas ya
Ivory coast ambako alidumu kwa miaka zaidi ya saba baada ya kuajiriwa 01/09/2003
mpaka 2009 kabla ya kuelekea Stade Tunisien.
Kabla ya
kuja barani Afrika alikuwepo Uarabuni kuanzia 01/07/2001 mpaka 29/08/2003.
Historia yake
ilianzia kuifundisha Paris Saint-Germain kama kocha msaidizi kwa kipindi cha
mwaka mmoja kuanzia 01.07.1999 mpaka 30.06.2002 kabla ya hapo akiwa katika
kipindi cha kujifunza zaidi akiwa kama meneja wa daraja la chini 01/07/1989
mpaka 30/06/1999.
Pia amewahi
kuzifundisha USM Malakoff ya Paris na Al
Wahda Club ya Abu Dhabi.
Uchunguzi wa Rockersports umebaini kuwa kocha Patrick Liewig ambaye ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 ni kocha mwenye wastani wa ushindi wa asilimia
30.77% sare asilimia 38.46% na kupoteza kwa asilimia
30.77%.
Katika
kipindi chake cha kuifundisha Asec Memosas amefainikiwa kuingiza timu hiyo
katika michuano ya vilabu bingwa Afrika mara saba na kufikia hatua ya nusu fainali
moja mwaka 2006.
Katika miaka
ya 2003, 2005, 2007 timu hiyo iliishia katika hatua ya makundi 2008 na miaka ya
2004 na 2009 aliisaidia kufikia hatua ya mzunguko wa pili.
No comments:
Post a Comment