Liverpool haitakutana na Gareth Bale wakati Real Madrid itakaposafiri kuelekea Anfield katika ligi ya mabingwa Ulaya lakini safu yake ya ulinzi haitakuwa na ahueni wakati mshambuliaji kinanda Cristiano Ronaldo atakapokuwa Atua uwanjani hapo.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United ameanza msimu katika uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu akifunga magoli mengi zaidi ya magoli yote yaliyofungwa na wachezaji wote wa Liverpool.
Katika michezo 12 ya kikosi cha Carlo Ancelotti Ronaldo ameshafunga jumla ya magoli 19 yakiwemo magoli manne mujarabu dhidi ya Elche, wakati ambapo wachezaji wote wa Liverpool wakiwa wametupia jumla ya magoli 17 katika jumla ya michezo 11
msimu huu.
Hiyo ina maana kuwa mreno huyo peke yake ameweza kufunga wastani wa magoli 1.58 kwa kila mchezo, wakati ambapo Mario Balotelli, Steven Gerrard, Raheem Sterling wakiwa na wastani wa magoli 1.54.
No comments:
Post a Comment