Kocha wa Manchester United David Moyes
ameonya kuwa timu yake bado inapaswa kupiga hatua zaidi baada ya kupata
uhai kidogo katika kinyang'anyiro cha kuwania kutetea ubingwa wake wa
ligi ya Uingereza Premier League, kwa kuishinda Arsenal jijini London hapo jana ambao
wanaongoza ligi hiyo kwa sasa.
Moyes ameshuhudia timu yake ikipata kipigo dhidi ya Liverpool, mahasimu
wao wakubwa Manchester City, na hata West Bromwich Albion tangu mwanzoni
mwa msimu, lakini ushindi wa bao 1-0 jana Jumapili dhidi ya
Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani Old Trafford umeiweka points
tano tu nyuma ya Arsenal.
Kipigo dhidi ya Man City na Tottenham Hotspurs mwishoni mwa juma ,
pamoja na sare ya Chelsea dhidi ya West Bromwich Albion, vimesaidia
Manchester United kujiweka miongoni mwa timu zinazowania ubingwa ,
lakini Moyes amesema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya.
"Itachukua muda kidogo kwangu mimi kuweka kila kitu katika mtazamo ninaoutaka".
Manuel Pellegrini kocha wa Man City amesema kikosi chake kinapaswa
kucheza vizuri zaidi ugenini iwapo kitawania nafasi ya kushinda ubingwa
wa Premier League msimu huu.
Kikosi cha Pellegrini kina rekodi safi sana nyumbani kikishinda michezo
mitano katika ligi hadi sasa msimu huu, lakini ugenini kimevurunda.
Licha ya kupata ushindi hivi karibuni ugenini katika Champions League na
kombe la ligi, City wamepata points nne tu katika jumla ya points 18
uginini katika ligi ya Uingereza baada ya kupata kipigo cha nne kwa bao
moja bila majibu dhidi ya Sunderland jana Jumapili.
No comments:
Post a Comment