Hapa akiwa bado katika uangalizi wa madaktari hospitali |
Hapa wakati akipiga samasoti yaani sarakasi |
Hapa ni wakati wa kuugwa mwili wa marehemu |
Mchezaji wa soka nchini India, Peter
Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya
kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo
alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya
kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu
yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa
kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema :
''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha
mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa
soka na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''
No comments:
Post a Comment