Bosi wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini ameripotiwa akiwaambia Tottenham kuwa anataka kuwa meneja wao mpya mwishoni mwa msimu.
Mancini ambaye kwasasa anaifundisha Galatasaray ya Uturuki inaarifiwa ya kuwa amekuwa hana utulivu mjini Istanbul, huku wengi wakitazamia kuwa huenda akaondoka wakati wa kiangazi.
Kwa mujibu wa taarifa nchini Italia zinaarifu kuwa bosi huyo mwenye umri wa miaka 49 yuko na mpango wa kurejea England na anafukuzia kazi katika klabu ya Tottenham.
Kwasasa Tim Sherwood ndiye anayekiongoza kikosi cha Totternham chenye maskani yake White Hart Lane na habari zinasema hatma yake ya baadaye itajadiliwa mwishoni mwa msimu huku mwenyekiti wa klabu hiyoDaniel Levy ameweka wazi kuwa upo uwezekano wa kumtafuta mbadala wake ambaye atatakiwa kuwa ni mwenye uzoefu mkubwa.
Meneja wa sasa wa Spurs Tim Sherwood |
Mancini inaamini kuwa tayari ameshawapiga maneno Spurs juu ya kutaka kazi hiyo huku mkurugenzi wa ufundi wa Spurs Franco Baldini akidai kuwa mwenyekiti Levy anafikiria sana juu ya meneja wa zamani wa City kuchukua nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment