KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 8, 2012

KIMATAIFA:Neymar azomewa na mashabiki wa Brazil, Joackim Low akasirishwa na ujerumani kushindwa kutumia nafasi ,Hodgson afurahishwa na Cleverly na Alex na Rijkaard anasema 'Sijawahi kuona timu nzuri ya taifa kama Hispania'


Neymar azomewa na mashabiki wa Brazil
Nyota wa Santos ya Brazi Neymar amesema hakufurahishwa na namna ambavyo mashabiki walivyo mchukulia kitabnia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao walipata ushindi wa bao 1-0 ambapo amewataka mashabiki kuifurahia timu yao badala ya kumnyooshea kidole mchezaji mmoja mmoja.
Neymar amewakosoa mashabiki wa taifa lake kwa kukosa uzalendo katika mchezo ambao Brazil maarufu kama Selecao ilipochomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Afrika kusini mchezo uliopigwa hapo jana.
Mshambuliaji wa Zenit St Petersburg Hulk, ambaye ndiye aliyepachika bao hilo tayari huko nyuma alikwisha wahi kutoa maneno kama hayo ya kuwakosoa mashabiki kuwa kwa kufanya hivyo wanawavunja moyo wachezaji.
Amenukuliwa Neymar akisema
"sisi wote tunajua kuwa hatukuwa katika kiwango kikubwa lakini tumefanikiwa kumepata ushindi. Nilijisikia vibaya sana kuona mashabiki wakituzomea , sitaki mashabiki wanipende mimi lakini waiunge mkono timu yao."
Mshambuliaji huyo wa Santos anadhani tabia ya mashabiki ya kukosoa ndani ya Estadio Cicero Pompeu de Toledo ilichangiwa na kuwepo makundi ya mashabiki toka katika timu kubwa hasimu nchini humo.
Ameendelea kunukuliwa kwa kusema
"sijui sababu hasa ya kuwepo na tabia hii kwa mashabiki , lakini inawezekana ikasababishwa na kuwepo na kundi kubwa la mashabiki katika vilabu vya Palmeiras, Corinthians na Sao Paulo.
"lakini narudia , wanapaswa kuiunga mkono timu kuliko kuizomea."
Mchezo unaofuata kwa Brazil ni dhidi ya China ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kiarafiki jumanne.


Joackim Low akasirishwa na ujerumani kushindwa kutumia nafasi
 Meneja wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amekasirishwa na vijana wake kwa kushindwa kuzitumia nafasi nyingi walizo pata katika mchezo wa kuwania kupata nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia licha ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya visiwa vya Faroe .
Mabao mawili ya Mesut Ozil na lingine la Mario Gotze yameipa Ujrumani points tatu muhimu na kukalia usukani wa kundi la C.
Amenukuliwa Low akisema
"ni wazi tangu mapema tulikuwa na nafasi ya kufunga lakini tatizo letu ni kupoteza nafasi na si katika mchezo huu pekee"
Mchezo huo haukuwa mchezo mgumu kwa Ujerumani ambayo baadaye itakutana na Sweden na Austria katika michezo mingine ya hatua ya makundi kusaka nafasi tya kucheza kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Ameongeza  Low akisema
" Faroe si kipimo kwa Ujerumani kwa timu nyingine tutakazo kutana nazo katika kundi".


Hodgson afurahishwa na Cleverly na Alex
 Meneja wa England Roy Hodgson amesema amefurahishwa na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Moldova.
Mbali na hilo amepongeza uwezo wa vijana wake chipukizi katika timu ya taifa Tom Cleverley na Alex Oxlade-Chamberlain hasa katika mchezo wa jana wa kuwania kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia dhidi ya Moldova.
Cleverly wa Manchester United na Oxlade-Chamberlain wa Arsenal wote walikuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha England ambacho kilipata ushindi mkubwa kuwahi kuwata huko nyuma tangu mwaka 1993 na kumpendezesha meneja wao ambaye amekuwa katika kipindi kigumu cha kujenga upya kikosi kwa ajili ya fainali ya kombe la dunia 2014 mwaka Brazil.
Hata hivyo walionekana kufunikwa na mkongwe Frank Lampard, 34, ambaye alifunga magoli mawili ya mwanzo huku Hodgson akiwataka vijana hao kuongeza juhudi kuwapiku wakongwe.
Amenukuliwa Hodgson akisema
 "kwa kweli nimefurahishwa sana na Tom na Alex, imedhirisha sasa kwanini Sir Alex Ferguson anamtumia katika timu yake”.
Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na Jermain Defoe kabla ya mapumziko na mengine yaliwekwa nyavuni na James Milner na Leighton Baines.


Rijkaard: Sijawahi kuona timu nzuri ya taifa kama Hispania 
 Kocha wa timu ya taifa ya Saudi Arabia Frank Rijkaard amepaza sauti na kusema anazimika sana na timu ya taifa ya Hispania hii ikiwa ni kauli iliyokuja baada ya kuchakazwa kwa mabao 5-0 hapo jana Friday.
Mabao ya Santi Cazorla na Pedro yaliwapa uongozi wenyeji kwa mabao 2-0 kabla ya mapumziko na baadaye Xavi, David Villa na Pedro yakakamilisha idadi ya mabao 5 na ndipo Rijkaard aliposema anaipongeza Hispania ‘La Roja’ kwa kiwango safi.
Amenukuliwa akisema
"timu ya taifa ya Hispania inavutia dunia nzima , na sijawahi kuona timu ya taifa yenye ubora kama Hispania.
"Xavi na Andres Iniesta ni miongoni mwa wachezaji bora duniani, wanaweza kucheza kwenye timu yoyote.

"Hispania ina kila sababu ya kutufunga. Wanatengeneza nafasi . sote tulijua toka mapema utakuwa ni mchezo mgumu. Tumecheza na timu dunia na hayo ni matokeo sahihi."
Hispania itaanza kampeni zake za kucheza kombe la dunia jumanne kwa kukutana dhidi ya Georgia.
 

No comments:

Post a Comment