KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 29, 2013

SIR ALEX FURGUSON ANAMTAKA KIUNGO WA KIMATAIFA WA KENYA.

Manchester United imetenga pauni pauni milioni £8 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Celtic na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.

Licha ya kwamba Celtic inaonekana kutokuwa tayari kumtoa kiungo huyo kwa kuwa bado ni muhimu kwao kutokana na ukweli kwamba alifunga goli goli muhimu la ushindi wa nyumbani katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona, bado United inaonekana kudhamiria kunasa saini ya kiungo huyo.

Uwezo wa Wanyama umevutia vilabu mbalimbali katika miezi ya hivi karibuni na vilabu vingi vinaonekana kufungua mazungumzo na mabingwa hao wa soka wa ligi ya Scotland na mchezaji mwenyewe huku United wakionekana kuwa tayari kufanya hivyo kwasasa.

Sir Alex Ferguson alimuona Wanyama wakati wa mchezo ambao Celtic ilishinda kwa mabao 4-0 katika dimba la nyumbani dhidi ya Dundee United wiki iliyopita.

Kama hiyo haitoshi kinachoonekana sasa ni kwamba kiungo huyo anaangaliwa kama kama chaguo muhimu la kuziba nafasi ya mchezaji mwingine mlengwa ambaye mipango ya United  kunasa imeonekana kushindwa, huyu si mwingine bali ni kiungo wa PSV Eindhoven Kevin Strootman.

No comments:

Post a Comment