David Beckham ameanza kufanya mazoezi na timu ya Arsenal leo wakati ambapo hatma yake ya baadaye katika soka ikiendelea kuwa kitendawili.
Nahodha huyo wazamani wa England mwenye umri wa miaka 37, amejiunga na washika mitutu hao kwa lengo kujiweka fiti wakati huu ambapo akili yake ikiendelea kusugua juu ya mwelekeo wake wa baadaye kufuatia kuondoka LA Galaxy mwishini mwa msimu wa ligi ya Marekani MLS mwezi December.
Karibu Beck: David Beckham akiwa katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal kwa mara ya kwanza akifanya mazoezi na wachezaji wa timu hiyo.
Beckham alionekana Hertfordshire akifanya mazoezi na kutania na wachezaji kadhaa akiwemo Jack Wilshere, Lukas Podolski wengine wengi wa kikosi cha Arsenal. Alionekana akivalia vifaa vya Marouane Chamakh,
ambaye kwasasa amepelekwa kwa mkopo West Ham.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid anaonekana kama anao uwezo wa kuimarisha tena uwezo wake na kucheza soka katika kiwango cha juu.
Beckham aliwahi kufanya mazoezi na Arsenal mwaka 2008 na wapinzani wakubwa kutoka London ya Kaskazini Tottenham miaka miwili nyuma baada ya msimu wa MLS kumalizika.
Kwasasa n i mchezaji huru hivyo anaonekana kutokuwa na papara ya kuamua hatma yake ya baadaye kwakuwa anaweza kusaini hata baada ya durisha la uhamisho kufungwa.
Akiongea meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema amemwita Bekham ili afanye mazoezi ya kujiweka fiti hivyo ni kwa ajili ya mazoezi tu na kuondoa minong'ono kama anaweza kumsajili
Kikosi cha Arsenal kilichosheheni vijana hakina nafasi ya kumsajili mzoefu kama Beckham kwasasa.
Running man: Hapa alikuwa akifanya tangazo la adidas nchini Hispania jana kabla ya kuelekea England la leo kufanya mazoezi na Arsenal
No comments:
Post a Comment