KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 28, 2012

YANGA YATANGAZA KUWAACHA 10 WAKIWEMO MWAPE ASAMOAH NA KADO

Maproo Davis Mwape na Kenneth Asamoah wote wameachwa na Yanga

Wakati tarehe ya mwisho kwa vilabu vya ligi kuu kutangaza wachezaji wao itakao waacha ikiwa inaelekea ukingoni june 31 2012, klabu ya Yanga hii leo imetangaza kuwaacha jumla ya wachezaji 10.
Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na wachezaji wawili raia wa kigeni Davis Mwape raia wa Zambia na Kenneth Asamoah raia wa Ghana.
Asamoah ameachwa na Yanga baada ya klabu hiyo kuvunja mkataba wake ambao ulikuwa umebakia mwaka mmoja.
 
Wengine walioachwa ni pamoja na ndugu wawili Abuu Ubwa na Zuberi Ubwa ambao hawakuwa na msimu mzuri katika msimu uliopita ndani ya klabu hiyo.
Wachezaji wengine ni Godfrey Born , Julias Mrope , Iddi Mbaga , Atif Amour na Kiggi Mkasi.
Msemaji wa Yanga Luis Sendeu ameiambia Rockersports kuwa mlinda mlango Shabani Kado aliyejiunga na Yanga akitokea timu ya Mtibwa sasa anarejea katika timu kwa mkopo.
 
Katika usajili wake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kombe la Kagame Yanga imewasajili wachezaji kadhaa akiwemo
 
Kelvin Yondani Ally Mustafa Bartez toka Simba, Frank Dumayo toka JKT Ruvu,Nizar Khalfani  huru akitokea nchini Marekani ,Ladslaus Mbogo toka Toto Afrika ya Mwanza  na Simon Msuva toka Moro United.



No comments:

Post a Comment