KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 28, 2012

RUFAA YA MANJI:WAZEE WA YANGA WAIPIGIA MAGOTI TFF

Wanachama wa Yanga wakiomba dua kabla ya kumngoa Loyd Nchunga madarakani
Baraza la wazee wa klabu ya Yanga limelitaka shirikisho la kandanda nchini TFF kuitupilia mbali rufaa ya mtu kwa mujibu wa baraza hilo la wazee "anayejiita mwanachama" wa klabu hiyo aliyewasilisha rufaa ya kuwapinga wagombea wawili wa uongozi ndani ya Yanga kwa madai kuwa mtu huyo si mwanachama halali.

Akinukuliwa katika kipindi cha michezo na burudani cha Redio Uhuru hii leo katibu wa baraza hilo Ibrahim Akilimali amesema uongozi wa klabu ya Yanga mara baada ya kupata jina la mkata rufaa huyo wameshindwa kumuelewa kuwa mwanachama huyo ni wa kutoka tawi gani kwani hata baada ya taarifa za kuwa anatokea tawi la Yanga Magomeni bado jina lake limeshindwa kuonekana katika leja ya wanachama wa tawi hilo.

Akilimali amesikika katika kipindi hicho cha michezo akilitaja jina la mwanachama huyo ambaye wameshindwa kumuelewa kuwa ni Ishabakaki Luta ambaye amekata rufaa ya kuwapinga wagombea wawili Yusufu Manji ambaye anawania nafasi ya Mwenyekiti pamoja na Yono Kevela ambaye anawania nafasi ya makamu mwenyekiti.

Mzee Ibrahim Akilimali maarufu kama 'Abramovich' ameitaka TFF kupitia kamati yake ya uchagujzi ambayo sasa juu ya suala hili itaketi kama kamati ya rufaa, kutupilia mbali rufaa hiyo na kuruhusu uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Julay 15 kufanyika ukitanguliwa na zoezi la kampeni ambalo linatarajiwa kuanza Julay 3.

Ishabakaki Luta amempinga Manji kwa kutoa jumla ya sababu 14 ambazo kwa mujibu wa dodosa za hapa na pale ni pamoja na madai ya kwamba Yusufu Manji ni kiongozi anayeendesha migogoro isiyokwisha Jangwani na ni kiongozi aliyehusika katika hujuma zilizopelekea Yanga kufungwa magoli matano na mtani wao Simba mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu ulikwisha.

Yusuf Manji
Sababu nyingine ni kuwa Manji alikiri kuwa kampuni iliyoingia mkataba na Yanga kitu ambacho hakikustahili kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Sababu nyingine iliyonaswa ni kuwa Manji ni mmiliki wa kampuni ya Kagoda ambayo inahusishwa na ufisadi wa madeni ya EPA.

Sababu nyingine iliyonaswa ambayo Luta ameitoa ni kuwa hivi majuzi serikali ilitamka wazi kuwa Manji anadaiwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano katika eneo lake la biashara la Quality Group hivyo kama kashindwa kulipa kodi serikalini kwa faida ya nchi je anaweza kuwa kiongozi?
Kwa upande wa Yono Kevela Ishabakaki ameipinga kamati ya uchaguzi ya Yanga kumpitisha mgombea huyo kwani alishapoteza sifa ya kuwa kiongozi sababu ambayo pia imetumika katika moja ya hoja ya kumpinga Manji. 

Stanley Yono Kevela mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Yanga

Katika hatua nyingine wanachama wa klabu ya Yanga kesho watakutana katika  makao makuu ya klabu hiyo kwa lengo la kuomba dua kuwarehemu wazee walioitumikia kwa namna moja ama nyingine klabu hiyo katika miaka iliyopita hilo limethibitishwa na msemaji wa klabu hiyo Luis Sendeu ambaye amesema hitma hiyo itafanyika kuanzia saa saba mchana.

No comments:

Post a Comment