Super Mario Balotelli akipongezwa baada ya kufunga bao la pili la Italia |
Mario
Balotelli ameutaja usiku wa jana kuwa ulikuwa ni wa kipekee katika maisha yake
baada ya kuisaidia timu ya taifa lake la Italia kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi
ya Ujerumani ushindi ambao umekivusha kikosi cha kocha Cesare Prandelli kutinga fainali ya Euro 2012.
Balotelli alikuwa
katika usiku wa kipekee uliokuwa bora kimchezo katika maisha yake ya soka akiwa
amevalia jezi ya rangi ya blue akifunga mabao mawili la kwanza la kichwa
kufuatia kross ya Antonio Cassano na bao la pili baada ya kupokea pasi ya
kutanguliziwa na Riccardo Montolivo.
Mshambuliaji
huyo wa Manchester City amekuwa akiandamwa na vyombo vya habari katika fainali
hizi hususani baada ya kupigiwa kelele na meneja wake kuwa kiwango chake
kilishuka hususani katika mchezo mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Ireland.
Lakini baada
ya yote hayo jana alionekana akiwa na tabasamu ambalo huwa ni nadra kuonekana
hivyo baada ya mabao yake mawili kutosha kubariki safari ya Italia kucheza
fainali ya Euro 2012 baada ya kuikosa kwa miaka 12.
Amenukuliwa akisema
“huu ulikuwa
ni usiku wa furaha na aina yake katika maisha yangu lakini nadhani jumapili
itakuwa zaidi,”.
“natumaini
kushinda , sijali kama nilicheza vibaya kwa kuwa tulijituma . sasa tunapumzika
, hatupaswi kujichanganya kuhusiana na mchezo wa Hispania wa kutawala mchezo
sisi tunacheza mpira wetu.
Balotelli amesema
magoli aliyofunga yalikuwa ni maalum kwa mama yake ambaye alisafiri kutoka
Italia kwenda kuona mchezo huo.
“Baada ya
mchezo nilikwenda kwa mama ilikuwa rah asana nilimwambia mama haya ni kwa ajili
yake,” .
“nilikuwa
nasubiri kipindi kama hiki kwa muda mrefu ukizingatia mama yangu si kijana tena
hawezi tena kusafiri mbali kwa hiyo ilikuwa ni kumfanya mwenye furaha kusafiri
mpaka hapa. Baba yangu atakuwepo katika mji wa Kiev katika mchezo wa fainali.
“kabla ya
mchezo kulikuwepo mama yangu, kaka zangu,shemeji yangu na rafiki yangu kipenzi.
Ukaribu wao na mapenzi yao ni wazi viliniripua . Unajua nilikuwa nasikiliza
wimbo gani kabla ya mchezo? Drake. He’s
a friend of mine."
“Mwisho wa mchezo nilikwenda kwa mama
aaaaaaaaaah ilikuwa that was the best moment. Nilimwambia magoli haya ni kwa ajili yake”
hiyo ni kauli ya Mario Balotelli
Mabao ya Balotelli
ya jana yana muunganisha na wafungaji wengine wenye magoli mengi katika fainali
hizi Cristiano Rolando, Mario Mandzukic na
Mario Gomez lakini katika wote hao ni yeye aliyesalia katika mashindano.
Anaendelea kunukuliwa
akisema
“nitajaribu
kushinda tuzo ya mfungaji bora . katika soka mara nyingine unaweza kujaribu mara
nyingi na mambo yasiende kama unavyo tarajia na ukajaribu mara chache na
ukafanikiwa " .
No comments:
Post a Comment