Rais
mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi ameendelea
kupokea salamu za pongezi baada ya kushinda wadhifa huo katika uchaguzi
uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Salamu
nyingine za zimetoka kwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Sepp Blatter ambapo amempongeza Malinzi kwa kuchaguliwa na
kumtakia kila la kheri katika majukumu yake ya kuongoza mchezo huo
nchini.
Blatter
amesema ana uhakika ufahamu wake na uwezo wake katika uongozi ni muhimu
katika kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu nchini, na kuongeza kuwa
milango ya FIFA iko wazi wakati wowote anapotaka kujadili masuala
yanayohusu mchezo huo.
“Nakutakia
wewe na kamati mpya ya Utendaji iliyochaguliwa kila la kheri, nguvu, na
kila aina ya mafanikio kwa changamoto zilizo mbele yenu,” amesema Rais
Blatter katika salamu zake.
Wengine
waliomtumia Rais Malinzi salamu za pongezi ni Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya, Rais wa Heshima wa
Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa,
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) na Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arumeru (ADFA), Peter Temu.
No comments:
Post a Comment