KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 30, 2013

AMAVUBU NA UGANDA CRANES WAJIANDAA NA CHALENJI KWA KUKUTANA NOVEMBA 15.

Friendly Game:
Uganda Vs Rwanda (6 pm)
Friday, 15th November 2013
Nelson Mandela Stadium,
Kampala
Ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya michuano ya Chalenji ya CECAFA, na michuano ya CHAN 2014, shirikihso la soka nchini Uganda (FUFA) limeandaa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda maarufu kama Amavubi mchezo ambao utapigwa Ijumaa ya Novemba 15 katika jiji la Kmapla.

Timu hiyo ambayo imepata udhamini wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, inajaribu wachezaji wake ambao walikuwa mazoezini kwa wiki mbili chini ya mkufunzi wa Kisebia Milutin 'Micho' Sedrojevic.

Waamuzi kutoka nchini KENYA ndio watakao kuwa uwanjani kufuatia shirikisho la soka la Uganda kutuma maombi nchini Kenya kwa shirikisho la huko(FKF).

Mchezo wa mwisho kwa vikosi vya timu hizo kukutana ilikuwa ni katika mchezo wa kirafikia mwanzoni mwa mwaka ambao ulimalizika kwa sare ya bao 2-2 katika uwanja wa Amhoro mjini Kigali. 
Rwanda iko katika nafasi ya 129 kwa viwango vya FIFA wakati Uganda wakiongoza katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wakiwa katika nafasi ya 84.
Uganda inatazamaiwa kuelekea Nairobi Novemba 24 kabla ya kuanza kwa michuano ya Afrika mashariki na kati ya Chalenji kuanza Novemba 27.

No comments:

Post a Comment