Klabu ya Real Madrid imehifadhi taji la kuwa klabu
tajiri zaidi duniani kwa msimu wa tisa mfululizo, kuambatana na orodha
ya vilabu tajiri iliyochapishwa na kampuni ya uhasibu ya Deloitte.
Klabu nyingine ya Uhispania, Barcelona
inashilikia nafasi ya pili ikifuatwa na Bayern Munich ya Ujerumani,
katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.
Kwa mara ya kwanza klabu ya Manchester United
ambayo kwa sasa imekabiliwa na msururu wa matokea mabaya katika ligi kuu
ya Premier ya England, imeshushwa miongoni mwa vilabu tatu tajiri zaidi
duniani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.
Waandishi wa habari wanasema kuwa ligi ya vilabu
vingi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha, nyingi ya vilabu hivyo
vinaendelea kupata hasara kubwa kutokana na gharama za mishahara na
malipo ya usajili wa wachezaji.
Mapato ya jumla ya United yamepanda kutoka £323.7 mpaka £346.5 msimu uliopita lakini pamoja na ongezeko hilo bado imepitwa na Bayern Munich kupitia ripoti ya 'Deloitte Football Money League'.
Mafanikio ya Munich yametokana na mafanikio ndani ya 'UEFA Champions League' na mafanikio ya ndani ambayo yameisaidia kuongeza mapato kwa asilimia 17 mpaka kufikia £352.5.
Ripoti hiyo imevijumuisha vilabu vitano katika idadi 20 vya juu. Manchester United ya Sheikh Mansour imepanda mpaka nafasi ya sita katika orodha hiyo ikiwa ndio klabu ya juu zaidi kutoka 'Premier League' ambao wamewashinda Chelsea walioshika nafasi ya saba na Arsenal nafasi ya nane ikiwa ni kwa mara ya kwanza.
Tottenham imeendelea kusalia katika nafasi 14. Deloitte wanasema vilabu vya Uingereza kama Everton, Newcastle United,na West Ham United
vinaweza kutoa changamoto katika nafasi 20 bora za utajiri msimu ujao kwasababu ya ingizo la mpango mpya wa haki za matangazo katika Premier League.
Real Madrid inaongoza ligi hiyo ya ushindani wa kifedha 'money league' kwa karibu miaka nane mfululizo na kuwashinda matajiri wa miaka ya nyuma ambapo mapato ya Madrid yamefikia £424.2. Barcelona imeshika nafasi ya pili.
Austin Houlihan, meneja mkuu wa Sports Business Group wa Deloitte amekaririwa akisema"
Wakati Manchester United wakishuka kwa nafasi moja katika 'money
league', matangazo mengi ya kibiashara ya klabu hiyo yanatarajiwa kuinua kipato cha klabu hiyo katika kipindi cha msimu wa 2013/14, hivyo basi anguko hilo la mpaka nafasi ya nne huenda likawa ni la muda mfupi.
"mpango unajumuisha pia kuimarika kwa dili lao la matangazo la miaka mitatu katika Premier League kuazia msimu wa 2013/14, ikiwa ina maana kuwa wanaweza kukaribia euro €500m (£408.7m) mpaka kufikia mwaka ujao wa 'money league'.
"Ukiachilia mbali mpango huo wa mwaka 2013/14, kama wataendelea kufuzu katika Champions League hiyo itakuwa ni changamoto nyingine ya kurejea katika 'top spot' katika 'money league' ijayo, nafasi ambayo waliawahi kuichukua msimu wa 2003/04."
Dan Jones, mshirika katika 'Sports Business Group ndani ya Deloitte,amesema
"Real Madrid imesalia katika nafasi ya juu ndani ya 'money league' pamoja na kwamba klabu hiyo imeshindwa kupata mataji ya kutosha katika mwishoni mwa msimu wa 2012/13.
"Licha ya hali ngumu ya kiuchumi hususani ndani ya Hispania, uwezo wa vilabu kuongezea mapato katika mazingira ya ndani na nje limekuwa ni kikwazo kufikia mafaniko kwa Madrid. Hali hiyo imeendelea kupanua mwanya wa utofauti dhidi ya wapinzani wao wa karibu katika 'money league', FC
Barcelona, kiasi kufikia euro €36m (sawa na £29.4m)."
Katika hatua nyingine, Paris Saint-Germain imepanda mpaka kuingia katika tano bora. Mapato ya klabu hiyo yamefikia pauni milioni £326 tangu mwaka 2010/11, na imejumuisha mapato ya matangazo ya pauni milioni £208.2 ikiwa ni kiwango cha juu cha mapato kupitia matangazo kwa vilabu vya soka.
Houlihan ameongeza kwa kusema
"PSG ndio klabu iliyopanda kwa kasi katika 'money
league' na kudai kuwa ndiyo klabu iliyo katika nafasi ya juu kutoka Ufaransa.
Ndio wawakilishi pekee katika klabu 20 za juu.
"Tunatarajia kuwaona wakiwa ni wakazi wakubwa katika nafasi tano za juu katika miaka ijayo, ikiwa chini ya wamiliki kutoka Qatari na wenye sapoti kubwa ya matangazo.
"Usajili wa David Beckham katika nusu ya pili ya msimu wa 2012/13 ndiyo iliyokuwa chachu ya ongezeko kubwa na kuwa klabu yenye uwezo duniani.
Galatasaray na Fenerbahce ni vilabu kutoka Uturuki ambavyo vimetokezea katika 'money league',
kufuatia mafanikio katika kampeni za michuano ya vilabu barani Ulaya na kuwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005/06 na kwamba vilabu hivyo viwili nje ya tano bora ndani ya 20 bora.
No comments:
Post a Comment