Javier Hernandez akifunga goli la pili huku mpira ukionekana kumpita Adam Federici. |
Manchester United walilazimika kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha inalinda ushindi wake katika dakika kumi za kuelekea kumaliza kwa mchezo baada ya Jobi McAnuff kuifungia goli Reading katika dakika ya 81 ya mchezo wa hatua ya mtoano wa michuano ya FA ambapo United imeshinda kwa mabao 2-1.
Baada ya kukaliwa kooni hatimaye vijana wa Sir Alex Ferguson walifanikiwa kufunga goli la kwanza kunako dakika ya 69 baada ya Nani kuukwamisha mpira wavuni kufuatia pasi ya Antonio Valencia.
Javier
Hernandez alifunga goli la pili baada ya dakika tatu lakini McAnuff akaharibu utamu baadaye kwa kufunga goli kwa Reading na kufanya dakika kumi za mwisho mchezo kuwa mgumu
Nani akifunga goli la kwanza la Manchester United mchezo uliopigwa Old Trafford.
Sir Alex Ferguson akishangilia goli mbele ya mashabikiwa wa uwanja wa nyumbani.
Danny Guthrie akijaribu kumdhibiti Anderson.
.
Phil Jones akigumia maumivu kabla ya kutolewa kipindi cha kwanza.
Phil Jones akitolewa uwanja baada ya kupata majeraha.
Ferguson (kushoto) akiongea na mwamuzi wa akiba Phil Dowd wakati wa mapumziko.
No comments:
Post a Comment