KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 18, 2013

IDDI MTINGINJOLA AMZODOA LEORDIGAR TENGA AMWAMBIA KUWA HANA KANUNI YA KUPITIA MAOMBI YA REVIEW. HIVYO WALIENGULIWA AKIWEMO MALINZI NJIA NYEUPE KWENYE CAS.

 
Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF Iddi Mtinginjola amesema kamati yake haina mamlaka kikanuni kusikiliza maombi ya mapitio ya rufaa yaliyowasilishwa na waliokuwa wagombea mbalimbali walioenguliwa katika kinyanganyiro cha uchaguzi za TFF na Bodi ya ligi.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo katika ofisi za shirikisho la soka nchini amesema kuwa kamati yake imekosa kanuni ya kufanya mapitio ya maombi ya wagombea walioenguliwa na kamati yake.

Amesema kimsingi wao kama kamati wanao uwezo wa kupitia upya maamuzi yaliyofanywa na kamati yake na si kufanya hivyo kutokana na maombi ya watu.
 
Amesema ni kweli kamati yake ilipokea maombi ya watu sita ambao waliomba maaamuzi ya rufaa dhidi yao kupitiwa upya ambapo pia aliwataja watu hao kuwa ni pamoja na Jamali Malinzi, Faridi Salim Nahad, Hamadi Yahya, Mbasha Matutu , Eliudi Peter Mvela na Klabu ya Mtibwa Sugar.

Amesema wao kama kamati baada ya kupokea maombi hayo wamejiuliza kama wana mamlaka ya kufanya hovyo kwa kuwa wamepitia katiba na kanuni za uchaguzi kama inavyo takiwa na kwamba kazi za kamati yake zinapaswa kuzingatia katiba na kanuni walizo kabidhiwa siku walipozindua kamati hiyo.
Mtingijola amesema kanuni za uchaguzi ibara ya 12(14) inasema shughuli za kamati ya rufaa ya uchaguzi zitakuwa zinatumia kanuni za uchaguzi za TFF na kwamba kama vile haitoshi ibara ya 49(6)(b) ya katiba ya TFF inasema inasema maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi  yatakuwa yanawabana pande zote za waliohusika katika shauri na kwamba pili hayapashwi kurudiwa.

Amesema dhana ya mapitio mapya imetokana na sheria za mahakama za kawaida kama sheria ya mwenendo wa kesi za jinai ibara ya 78(33) kinavyosema mtu ana nafasi ya kuomb review endapo ataona kuwa hakuridhika na maamuzi ya kesi na hivyo basi unaweza kuomba mapitio mapya Review kwa hakimu yuleyule kupitiwa upya.

BOFYA CHINI KUMSIKILIZA MTINGINJOLA

1 comment:

  1. Hii ndio misimamo inayotakiwa kwenye soka la tanzania ili tusonge mbele.Enzi za ubabaishaji zimepita.Amos Makala,maulid kitenge,michael wambura ,dioniz malinzi na mtandao mzima wa malinzi kuingia ikulu ya tff wasubiri 2017 kwa kuwa wakati huo mtu wao atakuwa na uzoefu wa miaka mitano ingawa bado atakuwa na doa la kupinga waraka

    ReplyDelete