Nigeria imeichapa Ivory Coast iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa wa kutwa taji la matiafa ya Afrika mabao 2-1 na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo inafanyika nchini Afrika Kusini.
Hili ni pigo lingine kwa Didier Drogba na kikosi kizima kwani bado ndoto ya taifa hilo kubwa ya kutwa taji hilo inazidi kuyeyyuka kila mara.
Sunday Mba
alifunga goli la ushindi kunako dakika ya 78 na kuisaidia Nigeria kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali kwa mara ya sita ndani ya michuano 6 iliyopita.
Amekaririwa kocha wa Nigeria Steven Keshi akisema
'Wakati tunakuja hapa, hakuna mtu alyetupa nafasi, lakini vijana wangu wameonyesha hilo kuwa wanaweza.'
Akiwa na umri wa miaka 34 Didier Drogba hajashinda taji la mataifa ya Afrika.
Gervinho wa Arsenal juu na Ya Ya Toure.
kocha wa Nigeria Stephen Keshi.
No comments:
Post a Comment