Bosi wa Arsenal
Arsene Wenger amefurahishwa na kiwango cha soka kilionyeshwa na nyota wake mpya
Nacho Monreal katika mchezo ambao washika bunduki waliibuka na ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Stoke hapo jana.
Katika mchezo
huo Lukas Podolski alifunga goli pekee kunako dakika ya 78 ambalo limeifanya Arsenal
kujikita katika nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi huku Monreal akiwaonyesha
jitihada kubwa katika sehemu ya ulinzi kwa mara ya kwanza.
Mlinzi huyo
mpya alikuwa na muda mdogo sana wa kuzoea kikosi chake kipya akihitaji
kijigeuza kidogo tu na kufanana na aina ya uchezaji wa timu hiyo yenye maskani
yake Emirates kabla ya kuingia katika kikosi cha kwanza ambapo Wenger anaamini
ulikuwa ni usajili chanya kumpata mhispania huyo.
Amekaririwa akisema
kuwa pengine ingekuwa ni ngumu kwake kwani alikuwa anakutana na timu inayotumia
nguvu sana nay eye akitokea katika soka la Hispania lakini anadhani Monreal
ameweza.
"Jambo
linalo ridhisha ni kwamba Monreal amekuwa na mwanzo mzuri, kwa mchezaji
kuwasili jana na leo kuwa katika timu kwa ujumla alikuwa akiimarika kadri
mchezo ulivyokuwa unaendelea"
Dembele
akatishwa tamaa na kupata nafasi 4 za juu za msimu huu.
Kiungo wa Tottenham
Moussa Dembele amewaonya wachezaji wenzake kwamba wako katika hatari ya kuwa
nje ya nafasi nne za juu katika ligi kuu ya soka nchini England, na kusema labda
wabadilike na kurudi katika njia ya kusaka ushindi katika michezo inayoendelea ya ligi hiyo.
Amenukuliwa akisema
"Ukiangalia
timu tuliyonayo hatuna sababu ya kuogopa timu yoyote katika Premier League, lakini
tunakosa nafasi nyingi za kufunga, wakati mwingine tunapoteza points katika
mchezo ambao tulistahili kushinda, inachanganya sana. Tuliposhinda Old Trafford
msimu uliopita tulicheza mchezo mzuri sana.
Angalia sasa
Arsenal, Chelsea, Liverpool wanapoteza points tulipaswa kuwa mbele yao”
Michael Owen kukabiliwa na adhabu ya FA
Mshambuliaji
wa Stoke Michael Owen huenda akakumbana na adhabu ya chama cha soka nchini
England FA baada ya kuonekana akimfanyia kitendo kisichokuwa cha kiungwana kiungo wa Arsenal Mikel
Arteta.
Wawili hao
walikumbana katika harakati za kuwania mpira dakika za lala salama katika mchezo
uliomalizika kwa Arsena kuibuka na ushindi wa bao 1-0 hapo jana, ambapo Arteta alikwenda kumkabili Owen ambaye alimsukuma kwa nyuma.
Mwamuzi Chris
Foy hakutoa adhabu kwa ya kadi kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33
lakini kamera ilimuonyesha Owen akifanya kitendo hicho.
Hata hivyo
bosi wa Stoke Tony Pulis baadaye akikaririwa akisema
"Arteta
ndiye aliyemkabili ndivyo sivyo Owen na kwamba Michael hakufanya hivyo”.
No comments:
Post a Comment