Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche (wa pili kushoto) akikabidhi funguo kama ishara ya kukabidhi basi la Taifa Stars kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Leodgar Tenga (wa tatu kushoto) wakati Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhii basi hilo leo makao makuu ya TBL Jijini Dar es Salaam. |
Rais wa TFF, Leodgar Tenga akisaini mpira. |
Kocha wa timu ya Taifa Kim Poulsen akitia saini mpira uliokabidhiwa timu ya Taifa katika hafla ya kukabidhiwa basi kutoka kwa wadhamini wa timu hiyo mchana wa leo. |
Wakaguzi wa ukanda wa Afrika wa bidhaa bia ya Kilimanjaro.
Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa timu ya taifa ya (Taifa Stars) leo
wamekabidhi rasmi basi la timu hiyo lenye thamani ya zaidi ya million 200.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa bia ya
Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria
51, uwezo wa injini ni 300 HP Cummins na kumeza lita 800 za mafuta.
Kavishe alifafanua kuwa TBL limenunua basi hilo ikiwa ni
sehemu ya ufadhili kama ilivyoaishwa katika mkataba baina ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) na kampuni hiyo.
“Imeshatimia miezi 10 tangu TBL ilipoanza kuidhamini Taifa Stars na malengo yetu kama wadhamini ni kuiona timu ikipata matokeo mazuri uwanjani jambo ambalo tumeridhika nalo”Alisema.
Alisema kuwa TBL itaendelea kusaidia timu ya taifa na hivyo
kupandisha kiwango cha soka nchini ili baadae waweza kupata nafasi ya kushiriki
michuano ya Afrika na baadae kombe la dunia.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodegar
Chilla Tenga ameahidi kwa niaba ya shirikisho lake kulitunza basi hilo kwa mafanikio ya timu hiyo ya Taifa
ambayo kwa sasa inafanya vema katika michezo mbalimbali.
Tenga alisema kuwa ujio wa basi hilo ni ishara
nzuri ya kuifikisha timu hiyo kwenye mafanikio zaidi
No comments:
Post a Comment