Lionel Messi akifarijiwa na mlinzi wa Milan Philippe Mexes katika dimba la San Siro baada ya mchezo usiku wa jana baada ya Barcelona kuchapwa bao 2-0.
|
Kipingo cha Barcelona kutoka kwa AC Milan katika mchezo wa kwanza wa vilabu bingwa Ulaya kilikuwa ni cha mshituko mkubwa katika hatua ya mtoano ya 16 za mwisho kuelekea hatua nyingine ya robo fainali.
Mabao ya nyota wa wa zamani wa Portsmouth Kevin-Prince Boateng na Sulley
Muntari yamekiacha kigogo hicho cha Catalan kikiwa na mlima wa kupanda katika kipindi cha maandalizi yake ya wiki tatu kabal ya mchezo wa marudiano.
.Lakini pamoja na kipigo hicho cha mchezo wa awali bado haijalishi kuwa wameshindwa.
Kuna mifano michache katika historia ambayo inawapa matumaini mabingwa hao wa mwaka 2009 na 2011 zaidi kuhusu michuano ya EUFA mwaka 1996 ambapo Zinedine Zidane aliwapa nguvu Bordeaux ilipowatoa Milan kwa kuwafunga mabao 3-0 nchini Ufaransa kufuatiwa katika mchezo wa kwanza kufungwa mabao 2-0 nchini Italia.
Wafungaji wa Milan Kevin-Prince Boateng (kushoto) na Sulley Muntari wakishangilia.
Wakati huo bao la Didier Tholot ukijumlisha na mabao mawili ya kipindi cha pili ya Christophe Dugarry yaliondoa matumaini ya magoli mawili ya ushindi ya mchezo wa mkondo wa kwanza yaliyofungwa na Stefano Eranio na Roberto Baggio.
Hiyo ilikuwa ni mara ya mwisho kwa timu hiyo ya kutoka nchini Italia kushindwa kufaidika na ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 katika michuano ya vilabu Ulaya.
Zinedine Zidane (katikati) akifanya vitu vyake akiwa na Bordeaux katika mchezo dhidi ya Milan mwaka 1996
Rivaldo na Luis Figo wakiongoza kikosi cha Barca kilicho ichapa Chelsea 5-1 katika dimba la Nou Camp mwaka 2000.
Luis Figo
Itakumbukwa pia Barcelona walimaliza matumaini ya Chelsea ya kusonga mbele kufuatia kuichapa mabao 5-1 katika dimba lake la nyumbani Camp Nou katika hatua ya robo fainali mwaka 2000 baada ya kufungwa kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza uwanja wa Stamford Bridge.
John Terry na Frank Lampard wakishangilia ushindi wa Chelsea dhidi ya Napoli.
Didier Drogba akifunga na kushangilia katika dimba la Stamford Bridge katika ushindi wa mabao 4-1 msimu uliopita.
HUZUNI NCHINI HISPANIA
Barca wako katika hatari ya kutolewa wakati ambapo wapinzani wao wakubwa katika soka la Hispani Real Madrid
pia wakifuta jasho baada ya sare ya bao 1-1 mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester United.
Kwa mara ya mwisho timu zote Real Madrid na Barcelona kushindwa kuingia katika hatua ya timu nane za mwisho ilikuwa ni mwaka 2007, ambapo Milan ilitwaa taji baada ya kuichapa Liverpool katika mchezo wa fainali.
Kwa mara ya mwisho timu zote Real Madrid na Barcelona kushindwa kuingia katika hatua ya timu nane za mwisho ilikuwa ni mwaka 2007, ambapo Milan ilitwaa taji baada ya kuichapa Liverpool katika mchezo wa fainali.
Leeds United iliwahi kuifunga Stuttgart bao 4-1 mwaka 1992 kufuatia kupoteza katika mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-0, na Chelsea iliwahi kuifunga Napoli mabao 4-1 katika dimba la nyumbani kufuatia kufungwa ugenini 3-1 msimu uliopita kabla ya hatimaye kusonga mbele na kutwaa taji.
Arsenal, pia inaweza kuyageuza matokeo ya Jumanne ya kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Munich. Tatizo ni kwamba washika bunduki watakuwa ugenini katika mchezo huo wa marudiano jambo ambalo ni gumu katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya timu kupata matokeo mazuri ugenini katika hatua kama hii.
Miujiza:Arsenal na Celtic wanasubiri miujiza kufuatia vichapo vikubwa kutoka kwa Bayern na Juve.
No comments:
Post a Comment