Tusker Lager,ambao ni
miongoni mwa wadhamini wakubwa wa michezo katika ukanda wa Afrika mashariki na
kati jumanne hii wametangaza udhamni wao wenye thamani ya dolari za kimarekani USD 450,000 kwa ajili ya michuano ya Tusker Cup
ambayo imepangwa kufanyika katika jiji la Kampala nchini Uganda.
Baraza la vyama vya soka
Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limetangaza kuwa michuano hiyo itafungua
pazia November 24 katika uwanja wa taifa wa Mandela ,Namboole.
Michuano hiyo itafikia
kikomo December 8.Katibu wa Nicholas Musonye ambaye alielekea Kampala jana kwa
ajili ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya michuano hiyo.
Wakifungua udhamini wao huo
hapo jana katika Hoteli ya Serena jijini Kampala, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya
bia EABL Lemmy Mutahi amesema uamuzi umekuja kujaribu kuzisaidia timu za mataifa
ya Afrika Mashariki kwa ajili ya safari ya kuelekea kwenye fainali ya Kombe la
dunia 2014.
Amesema wadhamni wamefurahia
michuano hiyo kupelekwa nchini Uganda ambapo kwa mwaka huu wameongeza sehemu ya
udhamni wao kwa asilimia 5% ukilinganisha na mwaka jana.
Kwa upande wake Musonye amesema
udhamini huo utakuwa ni pamoja na mambo mengine ni malazi na usafiri wa ndege kwa timu shiriki. Kiasi
cha dolari za Kimarekani USD 60.000 zitakuwa ni zawadi ambapo mshindi atazawadiwa
dolari USD 30.000, na mshindi wa pili USD
20.000 wakati ambapo mshindi wa tatu atapata dolari za kimarekani USD 10.000
Musonye amesema pia michezo
yote itaonyeshwa na kituo cha television cha Super Sport.
No comments:
Post a Comment