Arsene
Wenger anaamini kuwa Arsenal inaweza kupigania mataji msimu baada ya kuwa
katika kipindi kizuri cha kuwa wachezaji wake muhimu ambao walikuwa majeruhi huko
nyuma.
Mfaransa
huyo tayari ana uhakika wa kupata huduma za wachezaji Lukas Podolski, Olivier
Giroud na Santi Carzola, na kizuri zaidi ni Robin van Persie kusalia katika
klabu hiyo licha ya taarifa za kutaka kuondoka kushika kasi.
Wenge mwenye
umri wa miaka 62 anashukuru maandalizi ya kuanza msimu kwenda vizuri lakini pia
katika hicho chote kikosi chake kuepuka kupata majehihi.
Anasema
kwasasa kikosi kiko tayari kukabiliana na chanagamoto za kuwania mataji ukilinganisha
na msimu uliopita.
amenukuliwa
akisema
"tuko
katika hali imara kuliko msimu uliopita ambapo tuliwapoteza Nasri na Fabregas ambao
waliondoka lakini zaidi ya hapo tuliwapoteza pia Diaby na Wilshere ambao
walikuwa majeruhi" .
"hivyo
tulipoteza wachezaji wanne wakati wa kuanza msimu tofauti na wakati
huu,tunataka kushindana na hiyo ndiyo nia yetu.
Wakala:Giuseppe Rossi huenda akasema
ndio kuelekea AC Milan.
Wakala wa
mshambuliaji wa Villarreal Giuseppe Rossi amethibitisha kuwa huenda
mshambuliaji huyo akaelekea kukubali kujiunga na AC Milan.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 msimu uliopita alikuwa katika msimu mbaya kufuatia
kusumbuliwa na msuli tangu mwezi October, na kuanza kusumbuliwa tena wakati
akirejea katika mazoezi akiwa na manyambizi hao wa manjano mwezo April.
majeraha
hayo yalimnyima nafasi ya kucheza msimu uliopita ambapo alionekana dimbani
katika michezo 14 tu ambapo Villarreal ilifikia katika hatua ya hatari katika
msimamo wa ligi ya La Liga mwezi May.
Licha ya
kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu bado vilabu mbalimbali vikubwa barani ulaya
viliendelea kumfuatilia ikiwa ni pamoja na Milan.
Wakala wake Federico
Pastorello amethibitisha kupitia Sky Sport 24 kuwa huenda mshambuliaji huyo
akaondoka katika klabu hiyo.
Mshambuliaji
huyo ameitumikia timu yake jumla ya michezo 192 tangu alipo jiunga nayo mwaka
2007 akitokea Manchester United.
Mwamuzi kuchukua hatua dhidi ya Luisao
Mwamuzi Christian
Fischer amesema atachukua hatua ya kumshitaki mchezaji wa Benfica, Luisao baada
ya kumsukuma mpaka chini katika mchezo wa jumamosi wa kirafiki dhidi ya Fortuna
Dusseldorf, ambao ulishindwa kuendelea.
amenukuliwa
akisema
"nilishtuka
sana kufuatia kitendo hicho"
Fischer mwenye umri wa miaka 42 alikuwa
akiongea na chombo cha habari cha nchini Ujerumani DPA hapo jana.
amesema
"katika
kipindi chote cha miaka 20 ya kuwa mwamuzi sikuwahi kufanyiwa kitu mbaya kama
kile hata katika ligi kuu ya Bundesliga."
Fischer
ambaye aligoma kuendelea kupiga filimbi katika mchezo huo uliopigwa Esprit
Arena baada ya dakika ya 38 ameliambia The Express kuwa atachukua hatua
kufuatia tukio hilo
"katika
kuthibisha kama ushahidi nina kipande cha rikodi ya TV. Luisao anaweza kusema
atakavyo .lakini ni kichekesho kwa kwa kuwa kila mtu ameona kilichotokea."
Mkurugenzi
wa habari wa shirikisho la soka la Ujerumani Ralf Koettker,amesema ni jukumu la
chombo cha kinidhamu cha Ureno kumuadhibu au kutokumuadhibu Luisao.
Italy dhidi ya England: mshambuliaji
wa Manchester City Mario Balotelli nje.
mshambuliaji
wa Manchester City Mario Balotelli ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa
ya Italy ambacho kitakuwa dimbani dhidi ya England jumatano nchini Switzerland kwasababu
ya conjunctivitis.
Matatizo ya
macho yalipelekea mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hakuwepo katika
kikosi cha Manchester City kilichocheza dhidi ya Chelsea katika mchezo wa ngao
ya jamii hapo jana .
katika
kikosi hicho mbali na Ballotel lakini pia hakuna mchezaji wa Juventus wala Napoli
ambaye amejumuishwa kwasababu ya uwakilishi wao katika vilabu vya jumapili
katika mchezo wa Supercoppa mjini Beijing.
Kocha Cesare
Prandelli ametaja wapya nane ambao hawakuwahi kuwemo kikosini akiwemo Stephan
El Shaarawy wa AC Milan.
Prandelli
pia kawapumzisha wazoeefu waliofungwa katika fainali ya Euro 2012 na Hispania goli
4-0 lakini akiwaongeza wachezaji wanne wa Atalanta ambayo imerejea ligi kuu Serie
A lakini pia wakiwemo mshambuliaji Manolo Gabbiadini,mlinzi Federico Peluso na
mlinda mlango Andrea Consigli wakiingizwa kwa mara ya kwanza kikosini.
Walinzi Mattia
De Sciglio na Francesco Acerbi ni miongoni wachezaji watano waliochaguliwa
katika kikosi hicho kitakachokuwa dimbani huko Berne.
Wengine ni
mlinda mlango wa Genoa Mattia Perin na kiungo wa Sampdoria Andrea Poli ambao
walikuwa kwa mkopo Inter Milan msimu uliopita.
Uefa yapunguza adhabu ya Terry
Shirikisho
la soka barani ulaya Uefa imepunguza adhabu iliyotokana na michuano ya vilabu
bingwa ya mlinzi wa Chelsea John Terry baada ya rufaa ta mchezaji huyo
kufanikiwa.
Taarifa ya
bodi ya uongozi ya Uefa kupitia mtandao wake imethibtisha kuwa adhabu hiyo imepunguzwa
kufuatia rufaa ya Terry ambapo badala ya kusimama michezo mitatu sasa atasimama
michezo miwili.
Taarifa hiyo
imesomeka
"Licha
ya mlinzi huyo wa kati kuwa bado amesimamishwa kwa michezo mitatu kwa michezo
ya vilabu ya Uefa sasa mchezo wa tatu umeondolewa ndani ya kipindi cha miaka
mitatu ya adhabu hiyo.
Mlinzi huyo
wa kimataifa wa England alipewa adhabu hiyo baada katika mchezo wa pili wa nusu
fainali dhidi ya Barcelona April 24 ambapo alimpiga buti Alexis Sanchez akiwa
hana mpira.
Adhabu hiyo
ilimkosesha mchezo wa fainali dhidi ya Bayern Munich na sasa atakosekana katika
mchezo wa Super Cup dhidi ya Atletico
Madrid August 31.
No comments:
Post a Comment