Klabu ya Simba ambayo ndiyo mwajiri
wa aliyekuwa kiungo wa klabu hiyo marehemu Mutesa Patrick Mafisango imetoa
ufafanuzi juu ya kutolewa nje kwa vyombo vya marehemu mafisango katika pango
lililoko maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Akiongea na Rockersports afisa habari
wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amekiri kuwa ni kweli vyombo vya marehemu
Mafisango vilitolewa nje ya nyumba aliyokuwa anaishi marehemu lakini hilo
halihusiano moja kwa moja na Simba kwasasa kwani wakati vyombo hivyo mpaka vinatolewa
nje tayari mkataba wa Simba na mwenye nyumba hiyo ulikuwa umemalizika tangu
mwezi wa june.
Kamwaga amesema tangu wakati huo
mkataba unamalizika pango hilo lilikuwa chini ya mdogo wake marehemu ambaye
amekuwa akiishi na mafisango tangu wakati marehemu akiwa katika klabu ya APR ya
Rwanda na baadaye Azam fc kabla ya kuichezea klabu ya Simba.
Amesema mdogo wa marehemu aliomba
kuendelea kusalia hapo na kuendelea kutumia vyombo vya marehemu Mafisango na
Simba kwa kutambua udugu na ukaribu wa wanandugu hao iliamua kumuachia vyombo
hivyo lakini kwa makubaliano ya kutokuendelea kulipa pango hilo mara baada ya
mkataba wa nyumba hiyo kumalizika mwezi wa sita.
Tangu wakati huo mdogo wake na
marehemu aliendelea kuishi katika nyumba hiyo na huku akiwakaribisha ndugu
jamaa na marafiki karibu saba ambao wote ni wa Congo DRC.
Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na
makubaliano mengine kati ya mwenye nyumba na wakongo hao ambao mpaka wanatupiwa
virago hakukuwa na malipo yoyote yaliyofanyika jambo ambalo limemfanya mwenye
nyumba huyo kushindwa kuendelea kutoa hisani.
No comments:
Post a Comment