Mwesigwa |
Uongozi wa klabu ya yanga umeshangazwa
na kauli ya mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage baada ya klabu ya Simba kushindwa
kumsajili mlinzi wa APR ya Rwanda Mbuyi Twite
Akiongea na Rockersports katibu wa
Yanga John Selestine Mwesigwa amesema mwenyekiti wa Simba Rage ameshindwa kufanya
usajili kwa kwenda na mfumo wa sasa wakati huu badala yake akitaka kusajili kwa
mlango wa nyuma.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwesigwa
amesema Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kumfuatilia Mbuyi Twite hata kabla ya
kuanza kumfuatilia Kelvin Yondani na Simba ndio waliokuwa katika mbio za
kuizunguka Yanga Jambo ambalo hata hivyo Simba imegonga mwamba.
Amemtaka mwenyekiti wa Simba awaambie
ukweli wanachama na wapenzi wa klabu yake kilichotokea na vipi wameshindwa
kumsajili mlinzi huyo raia wa DRC badala ya kutupa lawama kwa uongozi wa Yanga
na TFF.
Mwesigwa amesema ingekuwa Simba
imemsajili kweli Mbuyi Twite basi mfumo wa kuhamisha wachezaji wa komputer( transfer
management system (TMS) ) ungeonyesha na kukataa data za Yanga kumsajili lakini
Simba wakionekana kutokuwa na taarifa kupitia mfumo huo jambo ambalo mwenyekiti
wa Simba halifahamu na ameshindwa kulielezea hilo.
Katika hatua nyingine Mwesigwa
amesema Yanga haiko tayari kushughulikia madai ya Simba kurejeshwa pesa walizo
mpa mlinzi huyo kwani wao kama Yanga hawafahamu lolote juu ya hilo.
No comments:
Post a Comment