Galliani aomba yaishe
kwa Allegri
Rais wa AC Milan Adriano Galiani |
Makamu wa Rais wa AC Milan Adriano
Galliani jana alimpigia simu kocha wa kikosi chake Massimiliano Allegri kumtakia
kheri katika simu yake ya kuzaliwa katika jaribio la kurejesha amani baina yake
na kocha wa AC
Galliani aliondoka uwanjani akiwa
mwenye hasira na kuonekana kuchanganyikiwa katika mchezo ambao timu yake
ilifungwa kwa aibu mabao 5-1 na Real Madrid juma lililopita mchezo wa kirafiki
huku akimtupia lawama kocha Allegri akimkosoa kwa mabadiliko aliyofanya katika
kikosi chake kilichokuwa dimbani siku ya mchezo.
Akinukuliwa na Gazzetta dello Sport
amesema
“ukicheza na Real Madrid hupaswi
kufikiri ni mchezo wa kirafiki ”
“tulikuwa New York, mbele ya
watazamaji waliojaza uwanja macho yote yameelekezwa kwake na wengine wakiungana
kupitia luninga zao, Milan si timu inayocheza Serie D side."
Galliani alichukizwa na Allegri
kufanya maamuzi ya kubadili wachezaji tisa katika kipindi cha pili pale Yankee
Stadium hata kama upande wa pili kikosi cha Jose Mourinho kikibadili wachezaji 11.
“yalikuwa ni makosa makubwa na siwezi
kuvumilia hilo. I’m p****d off,”.
Kufuatia kutoa maneno hayo ya hasira
(wakongo wanasema kutomboka) kwa Allegri, Bosi huyo akatoa maneno ya kumfariji Allegri
na kurejesha mahusiano mazuri kwa kumtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa.
AC Milan inatarajia kuanza kampeni
yake taji la Italia Serie A August 26 wakiwafuata Sampdoria.
Ilanova afurahishwa kwa
kurejea Villa
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova |
Bosi wa Barcelona Tito Vilanova amepongeza
kitendo cha mchezaji wake David Villa kurejea dimbani vizuri akiwa ni
mshambuliaji ambaye amekuwa hafanyi makosa anapokuwa anapata nafasi ya kufunga
na amekuwa akisubiriwa kwa muda mrefu.
Villa amekuwa nje ya uwanja tangu
kuvunjika mguu katika michuano ya vilabu bingwa duniani dhidi ya Al Sadd mwezi December
mwaka jana lakini jana akarejea baada ya kuingizwa katika dakika ya 73 toka
katika benchi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Dinamo Bucharest.
Katika mchezo huo Catalans
waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 shukrani kwa magoli ya Lionel Messi na Ibrahim
Afellay huku kurejea kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Villa kukionekana
kama ahueni kwa kocha Vilanova.
Amenukuliwa Vilanova akisema
"mwaka jana tulimkosa sana kwa
kuwa ni mchezaji mzuri katika kufumania nyavu ni mchezaji muhimu katika kikosi,
nimeongea na daktari na wataalam wa viungo kabla ya mchezo dhidi ya Dinamo. Ni
muhimu kupata wachezaji waliokuwa majeruhi kama Villa.''
No comments:
Post a Comment