Kilabu ya Entente Satif kutoka
Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu bora barani Afrika kwa mara ya
kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda kilabu ya AS Vita Club kutoka
jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mabao ya ugenini kufuatia
sare ya 3-3 siku ya jumamosi.
Raundi ya pili ya fainali katika
uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku
sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza iliochezwa mjini
Kinshasa.
Setif ilianza kuona lango na wapinzani wao dakika nne
katika kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye alifunga bao
kupitia pasi ya El Hadi Belameiri.
Lakini wageni hao walisawazisha
dakika tano baadaye kupitia Lema mabidi aliyepiga mkwaju kutoka nje ya
eneo la kupigia penalti ili kuimarisha matumaini ya timu yake.
Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.
Bao
hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha mchezo
mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia mbinu
chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka mchezo huo
kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.
No comments:
Post a Comment