KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 15, 2012

CIRCKOVIC: TIMU IMEANZA VIZURI, WACHEZAJI WAENDELEE NA NIDHAMU HIYO YA MCHEZO

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akikokota mpira huku mchezaji wa Jacob Massawe akimnyemelea wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi ambapo Simba ilishinda bao 3-0. 


Ligi kuu ya Tanzania Bara imeanza hii katika viwanja saba tofauti hapa nchini , ambapo mabingwa watetezi wa taji, Simba walikuwa katika uwanja wa taifa ikifungua pazia la ligi dhidi ya Afrikan Lyon imechomolza na ushindi wa mabao 3-0.
Simba imepata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji hatari Emmanuel Okwi bao lililopatikan katika kipindi cha kwanza kabla ya bao la pili kuwekwa wavuni na mlinzi wa kulia Nassoro Cholo.
Bao la tatu lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia kwa njia ya penati baada ya walinzi wawili wa Lyon kumkwatua Emmanuel Okwi katika eneo la hatari na bao hilo kuzamishwa wavuni na mshambiliaji Daniel Akufor.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Simba Milovan Circkovic amesema ameridhishwa na kiwango cha timu yake huku akipongeza kikosi chake kwa kuanza ligi hiyo na matokeo hayo.
Amesema anatarajia nidhamu ya kimchezo iliyoonyeshwa na kikosi chake itaendelezwa katika mchezo unaofuata ambao Simba itakuwa ikicheza dhidi ya JKT Ruvu mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Taifa.
Matokeo mengine mabingwa wa kombe la Kagame Yanga wamekwenda sare ya bila mabao 0-0 na Tanzania Prisons mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine pale mkoani Mbeya.
Saidi Bahanuzi wa Yanga akikabiliwa vikali na mlinzi wa Tanzanian Prison katika mchezo wa ufunguzi wa pazia la ligi kuu Tanzania Bara baina ya timu hizo mchezo uliomalizika kwa matokeo ya bila kufungana katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mkoani Mbeya.
MATOKEO MENGINE
Yanga  0 vs 0 Tanzania Prisons
Simba 3 vs 0 Afrikan Lyon 
Mgambo JKT 0 vs 1 Coast union
Toto Afrikan 1 vs 1 JKT Oljoro
Kagera Sugar 0 vs 1Azam fc
Ruvu Shooting 1 vs 2 JKT Ruvu
Polisi Moro 0 vs 0 Mtibwa Sugar

 RATIBA MZUNGUKO WA PILI

2 19.09.2012. 8 JKT RUVU  SIMBA NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM
19.09.2012. 9 MTIBWA SUGAR  YANGA JAMUHURI MOROGORO
19.09.2012. 10 AFRICAN LYON  POLISI MOROGORO AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM
19.09.2012. 11 RUVU SHOOTINGS MGAMBO JKT MABATINI PWANI
19.09.2012. 12 TANZANIA PRISONS COASTAL UNION SOKOINE MBEYA
19.09.2012. 13 KAGERA SUGAR JKT OLJORO KAITABA KAGERA
19.09.2012. 14 TOTO AFRICANS AZAM CCM KIRUMBA MWANZA

























































No comments:

Post a Comment