Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youiquing akumuonyesha
waziri wa habari utamaduni na michezo wa Tanzania Dr Fenera Mukangara jinsi ya
kupiga moja ya vifaa vya ngoma za
utamaduni .
|
Balozi wa china nchini Tanzania Lu Youiquing hii leo
amemkabidhi vifaa mbalimbali vya ngoma, muziki na filamu waziri wa habari,
utamaduni na michezo katika Dr Fenera Mukangara kwa lengo la kuimarisha
mahusiano katika nyanja za kitamaduni na filamu nchini.
Akiongea wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Balozi
Lu Youiquing amesema vifaa hivyo mbali na kuendeleza sekta nzima ya burudani
lakini pia vifaa hivyo vitasaidia kupunguza gharama za utayarishaji wa muziki
na uhariri wa picha za filamu kwa wadau wa tasnia hizo.
Kwa upande wake Dr Mukangara amesema wamepokea vifaa vingi
ikiwemo ngoma, magitaa na vifaa vingine ambavyo ni adimu nchini ambavyo
vitaimarisha ubora wa filamu.
Amesema huo ni muendelezo wa mashirikiano na Uchina katika
mipango mbalimbali ya kukuza sekta ya ngoma, muziki na filamu.
Dr Fenera amesema baadhi ya vifaa vitapelekwa chuo cha sanaa na vingine vitapelekwa katika kitengo cha filamu kwa kuwa kuna baadhi ya vifaa ni kwa ajili ya kufanyia editing.
Dr Fenera amesema baadhi ya vifaa vitapelekwa chuo cha sanaa na vingine vitapelekwa katika kitengo cha filamu kwa kuwa kuna baadhi ya vifaa ni kwa ajili ya kufanyia editing.
BOFYA CHINI
No comments:
Post a Comment