David Luiz, ambaye
alifunga goli la ufunguzi la Chelsea katika mchezo ambao timu hiyo iliibuka na
ushindi wa 6-1 mchezo wa ligi ya
mabingwa barani Ulaya dhidi ya Nordsjælland kule darajani, amesema klabu yake
itayachukuliya mashindano ya ligi ya Ulaya(europa league) kwa uzito mkubwa .
Ushindi dhidi
ya Nordsjælland ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha Rafael Benitez ambapo
David Luiz anasema,
"ulikuwa
ni mchezo mzuri kwa wachezaji wote kimorali, ubora na ufungaji wa magoli jambo
ambalo ni zuri katika siku zijazo.
"Tuna
kocha mpya na ana filosofia mpya jinsi tutakavyokuwa wepesi wa kumfuata
tutakuwa na timu nzuri"
No comments:
Post a Comment