Rafael Nadal amepiga hatua nyingine kuelekea kurejea katika namba moja ya ubora wa mchezo wa tenis baada ya kupata ushindi wake kwa shida dhidi ya Philipp Kohlschreiber katika michuano ya tenis ya China
Open.
Nadal mwenye umri wa miaka 27 raia wa Hispania alishinda kwa seti 6-4 7-6 (7-3) na kutinga hatua ya robo fainali ambapo atakuwa akikabiliana dhidi ya mtaliano Fabio Fognini wa Beijing.
Nadal atakuwa anachukua nafasi ya Novak Djokovic
kushika namba moja endapo atafanikiwa kuingia katika fainali ya michuano na endapo Msebia Novak atashindwa kutwaa taji.
Nadal alimchapa Kohlscreiber wakati walipokutana katika michuano ya US Opens."
No comments:
Post a Comment