KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 6, 2012

SENTONGO NA OKWI WAINYONGA KILI STARS. FAINALI YA TUSKER CHALLENGE 2012 NI KAMA 2008. KILIMANJARO NA ZANZIBAR KUKAMUANA WENYEWE KWA WENYEWE NAFASI YA TATU.


 Mabao mawili ya Robert Ssentongo na moja la mshambuliaji nyota wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi hii leo yamefanikisha kuwapa nafasi timu ya taifa ya Uganda “Uganda Cranes” nafasi ya kucheza fainali ya Cecafa Tusker Cup 2012 baada ya kuichapa Kilimanjaro Stars mabao 3-0 mchezo uliochezwa katika dimba la Mandela ulioko katika kitongoji cha Namboole. 
The Cranes ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 7 kwa bao zuri la mshambuliaji Emmanuel Okwi.

Mshambuliaji huyo wa Simba alipiga shuti mpira umbali wa mita 6 kutoka katika lango la Kilimanjaro baada ya kupokea mpira wa kupenyezwa kutoka kwa Denis Guma .

Kipindi cha pili Uganda Cranes iliendelea kulishambulia lango la Kilimanjaro na kutawala mchezo na kufanikiwa kuandika bao la pili kupitia Robert Ssentongo kunako dakika ya 53 baada ya kupokea pasi ya Godfrey Walusimbi.

Mshambuliaji huyo wa URA aliandika bao lake la pili na la tatu kwa Uganda Cranes kunako dakika ya 73 baada ya kumalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango Juma Kaseja uliotokana na shuti la adhabu la Moses Oloya.


Kwa ushindi huo wa Uganda sasa unarejesha kumbukumbu ya nyuma ya fainali ya mwaka 2008 ambapo walikutana na wapinzani wao wakubwa katika soka la Afrika Mashariki na kati.

Kwa upande waoTimu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Cup 2012 baada ya kuindosha kwa mikwaju ya penati 4-2 timu ya taifa ya Zanzibar baada ya dakika 90 za kawaida na baadaye kuongezwa dakika 30 kuhitimisha dakiak 120 za mchezo.
Ulikuwa ni mchezo wa funga nikufunge ambapo iliwachukua Zanzibar dakika 20 kuanza kuandika bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Khamis Mcha Khamis kabla ya Harambee kusawazisha dakika ya 30 kupitia kwa mlinzi nahodha Nadir ‘Cannavaro’ Haroub kuupiga kichwa mpira baada ya krosi ya uchonganishi ya Kevin Omondi akiwa karibu na Mike Barasa.

Zanzibar ilipata bao la pili kupitia penati iliyopigwa dakika ya 75 na Aggrey Ambrose Morris’ penati iliyotokana na nahodha wa Harambee Anthony Kimani kumuangusha katika eneo la hatari mshambuliaji Juma Jaku Juma.


Dakika tano baadaye mshambuliaji mkongwe Mike Barasa aliswazisha.

Katika hatua ya penati wachezaji Khamis Mcha Khamis na  Uthman Ali wa Zanzibar walikosa penati zao huku Mike Barasa, Joackins Atudo, Edwin Lavasta na Abdallah Juma wakifunga penati zao kwa upande wa Harambee licha ya Sabril Makame na Samih Nujju kufunga penati zao haikusaidia kutinga fainali.

No comments:

Post a Comment