TAARIFA KWA WANAYANGA.
Klabu ya Young Africans
ilikuwa ifanye mkutano Wanachama tarehe 08 Disemba 2013, kama ilivyokua
imetangazwa na Uongozi hapo awali. Tunapenda kutoa taarifa kuwa tarehe
ya mkutano huo sasa imebadilishwa na kusogezwa mbele hadi tarehe 19
Januari 2013 kwa sababu zifuatazo:
1.Kutoa nafasi kwa Wanachama na Wapenzi wa YANGA kushirki kikamilifu
maandalizi ya sherehe za Uhuru wa Taifa letu zitakazofanyika tarehe 09,
Disemba 2012, na
2.Tuko katika mazungumzo na Kampuni moja
maarufu ya kusimamia shughuli za mkutano huo kwa upande wa ufadhili, ili
kuweza kutunisha mfuko na Klabu kujiingizia mapato kati ya shilingi za
Kitanzania 200,000,000/= (shilingi milioni mia mbili tu) hadi
350,000,000/= (shilingi milioni mia tatu hamsini tu) na Kampuni husika
wameomba kuongezewa muda ili waweze kufanya hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Tunapenda
kuwashukru Wanachama na Wapenzi wa YANGA kwa mshikamano na umoja
uliopo. Tuzidi kuijenga Yanga kwa maendeleo na mafanikio daima.
"YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO"
YUSUF MEHBUB MANJI
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
No comments:
Post a Comment