Mlinzi wa Arsenal
Bacary Sagna amedai kuwa amekuwa na furaha kuichezea klabu yake hiyo akiondoa
uvumi ulionea kuwa ni miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa ambao huenda akaondoka
katika klabu hiyo baada ya mazungumzo ya mkataba wake mpya.
Sagna mwenye
umri wa miaka 29, alikosekana katika sehemu kubwa ya michezo ya msimu uliopita akisumbuliwa na matatizo ya mguu na sasa akisaka
mkataba mpya Emirates wakati huu ambapo mkataba wake wa sasa ukitarajiwa
kumalizika mwak 2014.
Mfaransa
huyo ambaye anaelekea kujikwaa katika sera ya Arsene Wenger ya kutoa mkataba wa
mwaka mmoja mmoja kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30 mwaka ujao,
aliripokuwa kuwa hana furaha na mpango uliopendekezwa kwake wa kuongezwa miezi
12 na kuongezewa mshahara wa pauni £60,000 kwa wiki.
Hata hivyo
Sagna amekanusha hilo na kusema kuwa yeye ni mwenye furaha ndani ya klabu hiyo.
"Nina
furaha. Ninafuraha kurejea uwanjani na kuichezea Arsenal, naangalia mbele
kucheza michezo mingi zaidi msimu huu kwa kuwa huko nyuma nilikuwa majeruhi''
FA kupigania dimba la Wembley kuandaa fainali Euro 2020
Mwenyekiti wa
chama cha soka nchini England David Bernstein amesisitiza kuwa dimba la Wembley
lazima liwe mwenyeji wa fainali za mataifa ya ulaya mwaka 2020 (euro 2020).
Bernstein amethibitisha
kuwa FA itaomba kuwa mwenyeji wa mchezo wa fainali na nusu fainali wakati ambapo Wales na
Scotland zimesema kuwa na mpango kama huo wa kuomba uenyeji na wakitaja jiji la Glasgow kuwa mwenyeji
wa mchezo wa fainali.
Wembley
utakuwa mwenyeji wa fainali ya ligi ya vilabu bingwa ulaya mwaka 2013 na Bernstein
anaamini uwanja huo utakuwa muafaka kuandaa fainali hiyo barani Ulaya.
"ni
wazi kabisa Wembley ni uwanja wa hadhi ya juu unapaswa kufikiriwa na UEFA na ni
jambo ambalo tutalipigia chapuo mapema.
Naye mtendaji
mkuu wa Wales Jonathan Ford amethibtisha kupeleka ombi lao UEFA wakitaka
michezo hiyo kupelekwa katika dimba la Millennium.
Deschamps huenda akasalia katika benchi la ufundi la ufaransa mpaka 2016.
Didier
Deschamps ni kama vile anataka kusalia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa mpaka
wakati nchi hiyo itakapo kuwa mwenyeji wa fainali za EURO 2016, ikiwa ni baada
ya mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa kuambiwa kuwa kimsingi hatafukuzwa kazi hata kama watashindwa kufuzu fainali
za kombe la dunia zijazo.
Wakati Ufaransa
ikiwa katika kundi moja na mabingwa wa Ulaya na Dunia, Hispania katika michezo
ya makundi kuwania kufuzu kombe la dunia, kocha huyo mwenye umri wa miaka 44
bila shaka hafarijiki na kauli hiyo na kwamba anachofanya ni kuhakikisha
anaziba mianya midogo midogo inayoweza kumtilia mashaka kibarua chake kwa kuhakikisha anafuzu fainali hizo za mwaka 2014
nchini Brazil.
Alipoajiriwa
mwezi July, Deschamps, ambaye alichukua taji la kombe la dunia kama mchezaji
akiwa na kikosi cha Ufaransa mwaka 1998, anasema huenda akajiuzulu kama
ataishindwa kulipeleka taifa lake katika fainali hizo.
Lakini Rais
wa shirikisho la soka la Ufaransa FA (FFF) Noel Le Graet amesema hakuna haja ya
kumuweka katika wasiwasi wa lazima afuzu kama tatizo ni hilo.
Amekaririwa Le
Graet akisema
"kama
tutafuzu kombe la dunia bila shaka Didier ataendelea mpaka 2016,"
"mkataba
uko wazi ni kwamba utaongezwa katika mazingira kama hayo".
Le Graet alimsainisha
Deschamps mkataba wa miaka miwili.
Amekaririwa akisema,
"hata
hivyo hata kama tukishindwa kufuzu jambo ambalo hatulitegemei kuondoka si jambo
la lazima. Kutakuwa na mazungumzo".
John Terry kukosa kombe la dunia la vilabu Japan.
Mlinzi wa Chelsea
John Terry huenda akawa bado hajaponya majeraha yanayo msibu ya msuli katika
kipindi klabu yake itakapokuwa na kibarua cha michuano ya kombe la dunia la
vilabu nchini Japan.
Mlinzi huyo
tegemeo Terry, ambaye kwasasa ana umri wa miaka 31, alipatwa na maumivu
alipogongana na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez katika mchezo
uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliopigwa Stamford Bridge mwezi
uliopita.
Meneja wa
muda wa klabu hiyo Rafa Benitez ameweka wazi hilo kwamba huenda akarejea katika
mchezo wa mwisho wa juma hili dhidi ya Sunderland, lakini bado hajarejea
sawasawa katika mazoezi na kuna mashaka kuwemo katika safari ya mashariki ya
mbali.
Jopo la
madaktari limemfanyia uangalizi mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England
hapo jana kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwemo safarini baada ya mchezo
dhidi ya Sunderland na wamekuwa na majibu ya mashaka.
No comments:
Post a Comment