Hamza Muwange |
Wakati michuano ya 36 ya kombe la chalenji ikielekea ukingoni huenga timu ya taifa ya Uganda (The cranes) ikamaliza michuano hiyo bila
ya kuruhusu nyavu zao kutikisika.
Wakati mlinda mlango nambari moja Abel Dhaira alipopatwa na majeraha katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Harambee Stars wadau wengi walidhani pengine mbadala wake Hamza Muwonge asingeweza kulinda lango la The Cranes kwa mafanikio kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo
mlinda mlango huyo amefanikiwa kudhihirisha uwezo mkubwa alionao baada ya
kucheza dakiki 348 bila kuokota mpira nyavuni.
Amenukuliwa kocha
wa The Cranes Bobby Williamson akisema
“hilo lilikuwa ni lengo langu, hakika
kimekazana mpaka limetimia"
Uganda na Kenya
zitakutana katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo kwa mara ya tatu tangu
mwaka 2008.
Amekaririwa mlinda
mlango Muwonge akisema
“tuna kikosi
chenye wachezaji wenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi ni matumaini tutashinda
mchezo wa fainali jumapili na kujilinda tusitie doa rekodi yetu”
Muwonge
analindwa na walinzi kama Guma Denis, Walusimbi Geoffrey, Isaac Inside na Henry
Kalungi ambao watataka kulinda goli lao lisichafuke.Uganda imetinga fainali za chalenji mara 18, na
kupoteza fainali 5 huku ikitwaa taji mara 12 mara ya mwisho kupoteza mchezo wa
fainali ilikuwa ni mwaka 1995 mbele ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment